Barua zilizokuwa zimetumwa kwa Rais Barack Obama na Seneta wa Mississippi Senator Roger Wicker zmebainika kuwa na sumu hatari aina ya ricin.Idara kuu ya upelelezi ya Marekani FBI imetoa taarifa hiyo na barua zilizotumwa kwa viongozi hao wawili zinahusiana.Barua hizo zote zilitumwa kutokea Memphis, Tennessee na mtu mmoja mwenye umri wa miaka 45 amekamatwa Mississippi kuhusiana na barua hizo.Pamoja na barua hizo, polisi mjini Washington wanavichunguza vifurushi vitatu wanavyovitilia mashaka vilivyogunduliwa katika ofisi za majengo ya seneti.Kugunduliwa kwa vifurushi hivyo kwenye eneo kubwa la majengo ya serikali kumesababisha wasiwasi na idara za usalama zimeongeza ulinzi.Barua kwa Rais Obama na Seneta Wicker zilitumwa kabla ya mashambulio ya mabomu mjini Boston.
story Credit: MO BLOG