
Ikiwa ni wiki ya tatu ya shindano linalowaunganisha waafrica kifikra kwa siku 91, tayari majina ya washiriki wa Ruby na Diamond house walio hatarini kutoka wiki hii yameshafahamika.
Angola ndio ambayo inapumulia mashine safari hii sababu washiriki wote wawili Biguesas na Neyll wamependekezwa kuchapa lapa. Nchi nyingine ambayo hata haijapumua baada ya mshiriki wake kuliaga shindano wiki ya kwanza ni Kenya, ambayo mshiriki wake Annabel ameingia katika kikaango cha biggie.
Washiriki wengine walioingia danger zone ni Natasha wa Malawi na Pokello wa Zimbabwe.
Katika orodha ya wiki hii Bolt wa Sierra Leone amepona kwa mara ya pili, wiki iliyopita alipendekezwa kutoka lakini aliokolewa na kipenzi chake Betty aliyekuwa HOH, na wiki hii amependekezwa kwa kura nyingi lakini ameokolewa tena na HOH wa Diamond Melvinopted na nafasi yake kupewa Annabel.
Picha za wahiriki waliopo kikaangoni
Pokello kutoka Zimbabwe
Neyll wa Angola
Beguesas wa Angola
Annabel wa Kenya
Natasha wa Malawi
