
Waandaaji wa reality show Big Brother msimu wa 9 maarufu kama hotshots wametangaza kwamba wamepata studio mpya inayofaa na kufanya show hiyo iendelee kama ilivyokuwa imepangwa.
Big Brother Hotshots ilihairishwa baada ya jumba hilo lililopo Sasani studio huko Johannesburg Afrika kusini kuungua moto na kutekeza vitu muhimu katika jumba hilo zikiwemo cameras.
M-Net na Endemol kutokana na tarifa waliyotoa Ijumaa, waandaaji walisema M-Net na Endemol SA walitumia saa 48 zilizopita kutafuta sehemu ambayo itafaa kufanyika show msimu huu wa 9 ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.
Baada ya kuchunguza uwezekano wote, timu imefurahishwa kutangaza kwamba show hiyo itaendelea kwa sababu sehemu ishapatikana kwa hiyo mwezi huu itaanza.
Vinginevyo, M-Net inawahakikishia mashabiki wa Big Brother kwamba show yao wanayoipenda itanza hivi karibuni, na wamewashukuru sana mashabiki wote kote barani Afrika kwa support yao walionyesha.
Siku rasmi ya kuanza Big Brother itatangazwa…
