
Kama ilivyo taratibu za mchezo wa Big Brother, kila mwanzo wa juma baada ya siku ya mtuano jumapili washiriki hupigiana kura za kutafuta nani wa kutoka kwa wiki inayofuata? leo zoezi hilo limefanyika huku Tanzania kupitia mshiriki wake Feza kuwa katika wakati mgumu baada ya mshiriki huyo kutangazwa kuwa Kikaangoni
Baada ya Biggie kutangaza watakao kuwa kikangoni kwa wiki hii ambao ni LK4 kutoka Uganda na Biguesas kutoka Angola,ilimtaka kiongozi wa nyumba ya Rubby Selly kutoka Ghana kumuokoa na kumuweka mshiriki mwngine kwenye kikaango ambapo alimuokoa Biguesas kutoka Angola na kumuweka Koketso kutoka Afika kusini.
Huku katika nyumba ya Diamond ikiwa Biggie aliwataja Hakeem kutoka Zimbabwe,Bolt kutoka sierra Leone,na Dillish kutoka Namibia.Hapo ndipo kiongozi wa nyumba Betty kutoka Ethiopia alipomuokoa mpenziwe Bolt kutoka Sierra Leone na kumuweka Feza kutoka Tanzania.
Hili linaonesha wazi kuwa mchezo unazidi kuwa mzuri maana Betty aamua kurudisha kisasi kwa Feza ambaye alimuweka katika kikaango wiki iliyo pita ila kwa bahati nzuri Waafrika walimuokoa kwa kumpigia kura za kubaki na kumfanya mshiriki Feza kutoka Tanznia kuwa mwenye wasiwasi mkubwa.
ili kumbakisha FEZA ndani ya nyumba hiyo ya kaka mkubwa Watanzania tunaoishi nchi mbali mbali za Afrika tujitahidi kumpigia kura muwakilishi wetu Feza ila aendelee kubaki ndani ya Jumba hilo
