katika hali ya kustaajabisha Africa mashariki yaonekana kuanza mchezo wa Big Brother vibaya baada ya washiriki wawili Denzel kutoka Uganda na Huddah kutoka Kenya kuyaaga mashindano hayo.
Denzel kutoka Uganda ndiye aliyekuwa mshiriki wa kwanza kutoka kwenye mjengo huo ambapo alifuwatiwa na Huddah kutoka Kenya ambaye alionesha kushangazwa sana na matokeo ya kura hizo kwani alionesha ni mwenye kujiamini kuendelea kuwepo katka mjengo huo wa Biggie.
Hata hivyo kibarua kilikuwa kigumu kwa kiongozi wa nyumba(HOH) Feza kutoka Tanzania ambapo mshiriki aliomweka kwenye kikango hakutoka na ndiye kiongozi wa nyumba(HOH)wa wiki ya kesho si mwngine bali ni Betty kutoka Ethiopia na hapo ndipo mchezoo unanzakuwa mtamu…….
Sambamba na hilo Biggie ameandaa mchezo ulioitwa ARROW ambapo washiriki waliotoka wanawapa kama task walioko ndani ya mjengo huo,hivyo mtangazaji IK aliwasomea baadhi ya task hizo ambapo Denzeli kutoka Uganda alichagua namba nne inayosema mshirii mmoja anatakiwa atembee na mikono na miguu akitoka nje, Denzel Alimchagua Nando kutoka Tanzania kuifanya Task hiyo kwa muda wa wiki nzima ,ikiwa Huddah kutoka Kenya alichagua task ya kwanza ilosema mshiriki atandike vitanda vya washiriki wote jumatatu na jumanne ambapo alimchagua Dillish kutoka Namibia.
Usiku huo ulishereheshwa na wasanii kutoka Uganda Radio&Weasle