Jumapili iliyopita Mshiriki Wetu kutoka Tanzania Feza Alinusurika kuyaaga mashindani ya Big Brother The Chace baada ya kuokolewa na Kura Tatu tu akiwa amemzidi kwa kura moja mpenzi wake Oneil kutoka Botswana Ambaye alimpita kwa kura Mbili Tu hivyo kuwa na kura chache zaidi zilizomsababishia kuyaaga mashindano hayo, Bimp wa Ethiopia Rafiki mkubwa wa Ammy Nando Kutoka Tanzania alionekana kung’ara zaidi baada ya kupata kura Kumi.
Kwa bahati mbaya mchezo ulivyo sasa Team Feza au Team Tanzania haina watu wengi sana ndani ya Nyumba kwasasa hivo kumfamya Feza wakati wote kuonekana kukalia Kuti Kavu.
Mara hii tena Feza amekuwa mmoja kati ya wale waliopata kura nyingi za kutoka, kutoka kwa washiriki wenzie huku Bevelly Kutoka Nigeria Ambaye ndio Head of The House Akimuokoa Bimp ambaye naye aliwekwa kikaangoni na badala yake kumtoka kafara Mrembo Dilish kutoka Namibia
Hivyo kuwafanya waliopo kikaangoni kuwa Cleo wa Zambia, Feza Tanzania na dilish Wa Namibia.
Kura za wana Afrika mashariki zinahitajika zaidi ili kumuokoa Feza ambaye zaidi ya kuwa muwakilizhi wa Tanzania lakini katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ni yeye tu aliyesalia