Mrembo Wa Ilala miaka iliyopita na mwanamuziki Feza Kessy Ambaye alikuwa ni moja ya Mtanzania aliyeiwakilisha Nchi Vizuri Kabisa katika shindano la Big Brother The Chase anatarajia kuwasili Kesho jioni saa 12:30 akitokiea nchini Afrika kusini na Ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini baada ya kutolewa Ndani ya mashindano hayo jumapili iliyopita ikiwa ni wiki mbili tu kabla ya mashindano hayo kumalizika
barbara Kambogi ambaye ni Meneja Uhusiano wa MaltChoice Tanzania Amewahimiza Watanzania wajitokeze kumpokea Mrembo huyo aliyewakilisha taifa katika mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka.
Baada ya kuwasili Feza atapata wasaa mdogo wa kuzungumza na waandishi wa habari na kupiga picha na washabiki wake watakaofika uwanjani kisha atapelekwa Hotel Kupumzika kabla ya kukutana katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi