
Motamma-Botswanna
Betty-Ethiophia
Jana haikuwa siku nzuri kwa nchi ya Botswana na Ethiopia baada ya kuwapoteza washiriki wake toka katika nyumba ya big brother, hata hivyo ilikua siku baya zaidi kwa mshiriki Bolt kutoka sierra leone Baada ya kuachwa mpweke na mpenzi wake betty ndani ya jumba hilo
Nando wa Tanzania aliyekuwa miongoni mwa washiriki 7 waliokuwa nominated, ndiye mshiriki aliyeokolewa na kura za nchi 5 za Afrika zikiwemo Kenya na Uganda (sasa nguvu ya East Afrika inaonekana).
Oneal wa Botswana ndiye aliyefuatia kwa kupata kura za nchi 4, akifuatiwa na Natasha wa Malawi kwa kura za nchi 3.
Kutokana na kwamba Bolt, Elikem and Betty walipata kura ya nchi moja moja, ilitumika sheria ya kuangalia mwenye asilimia ndogo zaidi kati yao ambaye aliibuka kuwa Betty ndiye atoke. Cha kushangaza Botswana haikumpigia kura mshiriki wao mwingine Motamma na kumfanya kukosa hata kura moja ya nchi yake, na badala yake waliamua kukusanya nguvu zao kumpigia kura Oneil ambaye kweli amefanikiwa kubaki.
Hivi ndivyo kura zilivyopigwa kwa washiriki wote 7
Angola: Oneal
Botswana: Oneal
Ghana: Elikem
Kenya: Nando
Ethiopia: Betty
Malawi: Natasha
Namibia: Nando
Nigeria: Nando
South Africa: Oneal
Sierra Leone: Bolt
Tanzania: Nando
Uganda: Nando
Zambia: Natasha
Zimbabwe: Natasha
Rest of Africa: Oneal
Total: Nando = 5; Oneal = 4; Natasha =3, Bolt = 1, Elikem = 1, Betty = 1, Motamma = 0. (Total: 15 Votes)
