Mkali wa muziki duniani, mwanamama Beyonce au mama Blue Ivy akiwa ni mtoto wake wa kike wa kwanza, ambae amemtaja kuwa ni mafanikio makubwa, katika vitu amevipata, mafanikio na kila, ila Blue Ivy mafanikio makubwa sana, alisema hayo wakati akiongea kwenye mahojiano.
Beyonce (34) alikuwa akipiga stories na magazine ya Garage kuhusu mambo yote ya umama, “wakati niliowahi kufurahia kwa kupata mafanio, ni wakati nilipojifungua binti wangu Blue Ivy” amesema Beyonce kwenye mahojiano hayo.
Beyonce pia anamsifia mama yake, amemshukuru mama yake kwa kumuamini na kufanya ndoto zake ziwe kweli. “Kila nachokijua kuhusu kuwa mama vinatoka kwenye mifano aliyonionyesha mama , mama yangu alifanya mimi na dada yangu tujiamini sana, na alitufundisha kila wakati kushukuru” Beyonce anasema.
Pia Beyonce amewatia moyo wasichana wadogo kuwatazama wanawake waliofanikiwa na kujaribu kufanya kazi kwa bidii na wao wafanikiwe.Beyonce ni mke wa rapper Jay Z kutoka Brooklyn, Marekani na ndiye baba Blue Ivy.