Kufuatia comments alizokuwa ametoa mkali Tyga mkali wa “Rack City” amesema lebo yake ilikuwa imemuweka tu kama mateka hawezi kufanya kitu na hakuna kitu kinachoendelea wakati albamu yake iko tayari lakini mambo hayaendi wala hakuna mpango wa kufanyika jambo, ndipo mkali huyo akamind akaanza kufunguka kwenye mitandao a kijamii.
Pia akatoa maoni yake juu ya Drake, rais wa Young Money/Cash Money Mack Maine ameonekana kujibu tweet hizo wiki iliyopita.
Mapema mwezi huu Tyga alitweet kwamba albamu yake ya Gold imeisha na akasema kwamba anaweza akaivujisha albamu hiyo yeye mwenyewe badala ya kusubiri siku maalum yya kutoka “Kiwanda cha muziki ni uwanja wa ushetani, mimi ni mtu waa Mungu” alitweet Tyga.
Tyga pia alisema hatakuwa sehemu ya Young Money kwa muda mrefu na alijibu moja kwa moja tweet mbili za Mack Maine.
Story kumuhusu Tyga iliyotoka online kupitia Vibe, Tyga alielezea kuhusu kutengana na Young Money.
“Naelekea kutengana nao, najaribu kuwa pekee yangu, hatuendi sawa na Drake kwa sasa, pia Nicki Minaj” alisema Tyga.
Tyga aliongeza kwamba hampendi Drake kama mtu, sio mkweli kwangu, napenda muziki wake, nadhani unaelewa nachokisema? Nadhani muziki wake ni mzuri, lakini mimi nay eye ni watu wawili tofauti, tulilazimishwa kuwa pamoja na ilikuwa kama tunalazimisha mahusiano kuwa pamoja. Ndivyo ilivyo, lakini nimekuwa marafiki na Chriss (Brown) kama miaka sita, huyo ndie rafiki yangu wa ukweli, kila wakati tuko pamoja” alisema Tyga.
Akaongeza wao hawafanyi muziki tu ila wanakuwa batani wakati wote, nadhani kuwa nimesaini Young Money, kila mtu alihisi kama walikuwa wakilazimisha mahusiano, sababu Wayne alituleta pamoja. Mwisho wa siku sababu kwanini nilisaini Young Money ni kwa sababu ya Wayne, sio kwa sababu ya Drake, sio kwa sababu ya Nicki, ilikuwa kwa sababu ya Wayne na mahusiano yangu na yeye”
Mack Maine Ajibu Comments Za Tyga Kuhusu Young Money
Related Posts
-
-
Msanii Mwingine Wa Muziki Bongo Fleva Afariki Dunia, Ni Wa Kundi La Tmk Wanaume Family
-
Picha: Mastaa watupu uzinduzi wa Tamthilia mpya ‘khona”, Itaonekana Dstv Hivi Karibuni
-
Video: Show Ya Miaka 13 Ya Lady Jay Dee
-
Mshiriki Wa Shindano La American Next Top Model Ya Tyra Banks Apigwa Risasi Nyumbani Kwa Boy Friend Wake
-
Kajala Atoa Ya moyoni baada ya kuchoshwa Na Uzushi wa Kuwa na Mahusiano na Mume wa Mtu
-
Kweli Kuzaa Kuzuri, Lupita Amkanyagisha Mama Yake Mzazi Ardhi Ya HollyWood