Uteuzi wa wajumbe wa kamati ya uongozi uliofanywa na mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mh Samweli Sitta umeibua mzozo na mabishano makali bungeni huku mmoja wa wateuliwa hao Mh. Profesa Ibrahim Lipumba akiukaata uteuzi huo kwa kile alichodai kuwa umependelea zaidi Chama cha Mapinduzi.
Mvutano huo umekuja muda mfupi baada ya mwenyekiti Mh Sitta kutangaza rasmi majina ya wenyeviti wa kamati zile 12 pamoja na uteuzi aliofanya wa wajumbe watano ambao wataungana na wale wenyeviti wengine kwa ajili ya kuunda kamati ya uongozi…,Baada ya uteuzi huo ndipo wajumbe mbalimbali akiwemo Profesa Lipumba waliposimama na kupinga uteuzi huo.