
Mivutano ya makundi mawili ya wajumbe wa bunge la katiba yanayobishania upiganaji wa kura ya siri au wazi yamesababisha kutoelewana na kukwama kwa muda kupitishwa kwa vifungu cha 37 na 38 kutokana na hofu ya baadhi ya makundi kuwa vifungu hivyo vinaweza kuwa na athari katika maamuzi kwenye bunge la katiba..,
Wakizungumza baada ya Mwenyekiti wa muda Pandu Kificho kutaka kuanza hatua za kupitisha rasimu hiyo, baadhi ya wajumbe wamemtaka mwenyekiti huyo kuahirisha vikao na wajumbe kurudi makwao mpaka kamati ya kanuni na maridhiano zitakapoafikiana badala ya kuendelea kupata posho ambazo ni kodi za wananchi..,
NB: kweli Hili ndio Lilikua Dhumuni la Bunge Hilo? Kwa hali hii inayoendelea huko bungeni ya mivutano isiyokuwa ya maana na wala haina tija kwa taifa je tutafika…????
