Chama cha Tennis Tanzania (TTA) kwa kushirikiana na Gymkhana Club ya Dar es salaam, leo wametengaza mashindano ya ya Tennis kwa vijana wa umri chini ya miaka 16 na wachezaji wenye ulemavu wa miguu yaani wheelchair.
Haya ni mashindano ya wazi na yanatoa pointi kwa wato watakao shiriki kwa kila kipengele cha umri (Age category) yani chini ya umri wa miaka 16, 14 na 12.
Pointi hizo zitatokana na wingi wa ushiriki au uchache wao, timu ambazo zimethibitisha kushiriki
mpaka sasa ni Kijitonyama Dar e salaam, Arusha, Morogoro na Baobab.
Mashindano yatafanyika kwa siku 2 siku ya Jumamosi 18 na Jumapili 19 Oktoba 2014.
Akizungumza Mkurugenzi wa Mashindano (Junior Championship) Fina Mango amesema bado wanahitaji wadau mbalimbali zikiwemo taasisi, mashule, na wadhamini ili kuweza kuwasaidi vijana ambao wangependa kucheza mchezo wa Tennis lakini hakuna fursa ya wao kucheza na kuonyesha vipaji vyao, ikiwemo ni haki pia ya msingi ya mtoto kushiriki katika michezo.
Mashindano haya yamedhaminiwa na kampuni ya Selcom Wireless Limited, ni kampuni iliyoanzishwa Novemba 2001, Akizungumza Meneja Mauzo Bupe Mwakalundwa amesema kampuni ya Selcom imeona kuna umuhimu mkubwa wa kudhamini mashindano hayo ili kuweza kuwapa vijana wadogo sehemu ambayo wataonyesha vipaji vyao na kushindana kwa nguvu ambapo baadae inatufanya kuweza kupata wachezaji wenye uzoefu na wanaomudu mchezo huo na kuupenda na kuwakilisha nchi pamoja na kuitangaza Tanzania katika michuano mablimbali mikubwa ya Tennis duniani.
Ameongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kudhamini mashindano hayo kila wakati pale inabodi kufanya hivyo hatimaye kuufikisha mchezo wa Tennis mbalimbali, katika mashindano hayo wapo watoto walemavu wanaotumia wheelchair, walemavu huwa wanasahaulika lakini Tanzania Tennis Association (TTA) iko nao pamoja nao watashiriki katika kucheza Tennis.
Kupitia huduma za Selcom Wireless Limited unaweza ukalipia huduma hapa nchini ikiwemo ving’amuzi mbalimbali, huduma ya M-Pesa, Luku, Usafiri na nyingine nyingi.