Mkali Chriss Brown jana Jumatatu asubuhi katika After Party ya BET 2014 alibebwa kutoka katika club ya Hollywood kuelekea kwenye gari ya mpenzi wake Karrueche Tran iliyokuwa ikimsubiri.
Tran mpenzi wake wanaoachana na kurudiana alikuwa akimsubiri Chriss Brown katika gari ya Orange tayari kumuondoa katika eneo la club hiyo, na haina shaka alipoingia kwenye gari hiyo alilala moja kwa moja kwa sababu alikuwa tipsy vyakutosha.Alikuwa ameshika na watu wawili mmoja upande wa kshoto na mwingine kulia huku waandishi kibao wakipiga picha na watu wakaribu wa Chriss Brown wakijaribu kuzuia kamera.
Chriss Brown aliperform mapema jioni katika tuzo za BET 2014 ikiwa ni show yake ya kwanza baada ya kutoka jela. TMZ katika ripoti yake ya nyuma iliripoti kwamba Chriss Brown aliahidi kubadilika baada ya kutoka jela ili asirudi tena jela.. Lakini mwenendo wake wa pale kwenye party bado kuna maswali kama anaweza kutimiza ahadi yake hiyo.