Muimbaji wa ngpma ya loyal mkali Chriss Brown ameomba msamaha kwenye mahakama baada ya kukutwa na kosa la shambulio alililolifanya huko Washington D.C, Chriss Brown amekutwa na kosa hilo jana Septemba 2 baada ya kumshambulia mtu mwezi Octoba huko Washington D.C.
Tukio hilo lilitokea wakati muimbaji huyo akiwa katika uangalizi kutokana na kosa la kumshambulia mpenzi wake waliokuwa wanaachana na kurudiana mwanadada Rihanna a.k.a bad gal Riri mwaka 2009.
Chriss Brown alipelekwa sehemu zakupewa ushauri na rehab mwaka huu, hilo lilisemwa na mwansheria wake Danny Onorato.
“Kusema hivyo tayari ameshaadhibiwa kwa makosa kama hayo yapo kwenye majalada” alisema mwanasheria wake kama ilivyoripotiwa na Associated Press kupitia ABC News.
Akizungumza Chriss Brown mwenyewe kuhusu swala hilo “Nitapenda kusema samahani kwa mahakama” alisema Chriss Brown.
Chriss anaweza kusamehewa kwa sababu alishakwenda jela kwa suala kama hilo, ingawa hili lakumshambulia mtu Washington D.C lilikuwa bado lijafikiwa maamuzi, lakini kwa sababu alishahukumiwa na akaenda jela kwa swala kama hilo anaonekana amekuwa na heshima hapo mahakama imemfikiria ndo maana hajatupwa nyavu tena.