
Mkali anayetokea Canada Justin Bieber amekamatwa nchini Canada baada ya kutokea ajali iliyohusisha ATV yake na minivan iliyokuwa ikiendeshwa na mwandishi wa habri na kwa sasa anashtakiwa na makosa ya kuendesha kwa hatari na shambulio la mwandishi wa habari TMZ imeeleza.
Bieber alipelekwa selo Ijumaa mchana huko PerthCounty Ontario, Polisi wamesema kulikuwa na majibizano kati ya Justin na mwanahabri huyo kwenye minivan baada ya kugongana.
Justin alipigwa picha akiendesha ATV akiwa na Selena Gomez Ijumaa iliyopita huko Ontario karibu na nyumbani kwa baba yake, Polisi wamesema Justin aliachiwa na atatakiwa afike mahakamani mwezi ujao.
Angeweza kupatwa na matatizo makubwa kwenye mikono yake, Justin kwa sasa yupo kwenye uangalizi kwa miaka 2, kufuatia kesi yake huko Los Angeles, kwa hiyo kunauwezekano mwaka kukamatwa huku kutaanzisha vurugu. Haya ndo yale yale ya Chriss Brown alikuwa under probation akafanya kosa, pia ndo yale yaliyokuwamkuta Meek Mill akiwa under probation akafanya kosa lingine ikawa probation violation ikampelekea kufungwa jela.
Mwanasheria wa Justin anasema justin na Selena wanatoa ushirikiano mkubwa kwa polisi katika uchunguzi.
Mpiga picha ambaye inasemekana alishambuliwa na Justin akishirikiana na mwanasheria wake anayeitwa Gloria Allred, mwanasheria huyo amsema tayari ameshawasiliana na Los Angeles Police Department LAPD.
Justin naye jela inanukia amekuwa akiandamwa na kesi kibao,juzi kati alisemekana walitoa rushwa kwa polisi ili rafiki yake akatize mpaka kuingia Canada akiwa hana valid docs na makosa mengine ambayo yamekuwa yakimuandama, ilisemekana alikuwa bado kwenye foolish age lakini kwa sasa Bieber is over 18, asipotulia jela inamuita. Haya ni maoni ya mwandishi kuelekea kwa Justin.
