Mshindi wa tuzo kibao, The Pos Star “New Flame” singer Chris Brwon mwenye umri wa miaka 26, amekwama kuondoka Phillipines kwa sababu ya mambo ya kimikataba kwenda mrama, imeripoti Phillipines News Agency Wednesday.
Brown alizuiwa kuondoka nchini humo masaa machache kabla hajatakiwa kuwepo Hong Kong kwa ajili ya show nyingine.
Taarifa kutoka kwa wakala zinasema, amri imetolewa na Phillipines Department of Justice Jumanne usiku kumzuia Chris Brown asiondoke nchini humo.
Usiku ule alifanya show kama ilivyokuwa imepangwa lakini ilitolewa amri ambayo ilimtaka Chris Brown awalipe pesa ambazo alilalamikiwa kuwa anadaiwa na kundi la dini nchini humo kwa kutokwenda kwenye show mwaka 2014.
Ripoti zilionyesha kwamba, msanii huyo ambaye anafanya vizuri kwenye charts mbalimbali alisema kwamba alishindwa kwenda kufanya show kwa sababu alipoteza passport yake.
Brown amekuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yake ya muziki, ikiwemo tuzo moja ya Grammy na tuzo tano za Billboards Musicm lakinia jamaa huwa anakumbwa na matatizo kinoma noma.