
Baada ya kuonekana mara nyingi sehemu mbalimbali ikiwemo usiku wa BET watu wengi wakawa wanajiuliza kuhusu Lil Wayne na Christina Millan, Je ni wapenzi? mambo yamekuwa wazi kwa sasa.
Christina Millan anasema hatimaye yuko na lebo yake, akaongeza yeye na Lil Wayne wanamahusiano, Wanafanya muziki pamoja, alionekana akisema hayo katika video iliyopostiwa na TMZ Julai 20.
Millan ambae amesaini lebo ya repa kutoka New Orleans ya Young Money Entertainment toka 2012, alifunguka akiwa njiani kueleka kwa Chriss Brown kwenye Celebrity Kickball game huko Glendale California.
Christina Millan na Lil Wayne walipigwa picha wameshikana mikono Julai 17 ilikuwa Alhamisi, ukiwaangalia tu kwa haraka haraka unasema mtu na mpenzi wake.
Ukweli utajulikana tu, Mapaparazi si ndo sisi, Millan yeye amesema mahusiano yao ni ya muziki kutokana statement yake….mengine mnayofikiria sio…
