Ilianza kama hutani, lakini sasa imeonekana kama Davido na Wizkid kuna ugomvi mkubwa unaendelea kati yao na ugomvi usiojulikana chanzo chake, nadhani mashabiki wao ndio waliosababisha ugomvi huo na mwisho wake na hivyo limekuwa beef kubwa.
Davido tayari ameshakuwa na mwaka wenye mafanikio , Wizkid hajawa na mafanikio sana lakini anaendelea kutoa hitz like it,s nothing.
Lakini toka Davido alivyoshinda tuzo ya BET tuzo ambayo Wizkid alishinda 2012, Watu Fulani hatimaye wameona Davido ameshamaliza smbscho snscho Wizkid, na anaweza kuchukua sehemu yake kama msanii mkubwa huku akiwa na umri mdogo zaidi.
Chakushangaza ni kwamba walionekana pamoja Marekani pamoja siku chache zilizopita wakionekana wenye furaha.
Wiki chache zilizopita Davido alimtakia Wizkid Birthday njema na hata kumuita “Oga” Nigeria lugha yao wenyewe wanaelewana what Oga means.
Baadhi ya Wanigeria wanatumaini ni stunt kama wasanii zisije zikawa zile za Tupac na Biggie, kwa saabu Davido anamashabiki wengi na alikadhalika Wizkid na huanza kupigana mashabiki hata kupelekea vifo.
Davido na Wizkid ni mastaa wakubwa nchini Nigeria wanatesa katika main stream huku wakiwa na mkwanja mrefu na wote wamefanya colabo kali nje ya Nigeria na wasanii wakubwa kutoka Marekani.
Kibongo bongo wasanii wawili ambao naweza kuwafananisha na Davido na Wizkid ni Ali Kiba na Diamond ambao pia ni wasanii wakubwa Tanzania, wote wakiwa na mafanikio sana ila mmoja amekuwa na mafanikio zaidi na mwenzake na kufanya colabo nyingi nje ya nchi na wasanii wakubwa.
Kulikuwa kama kuna kaugomvi lakini ni charasharasha kila mtu akiulizwa kuhusu mwenzake hataki kumuongelea, kuna stories ilishatoka kwenye tovuti moja Diamond alikaririwa akisema Ali Kiba anatafuta agombane nae ili Diamond ashuke yeye asonge mbele.
Kwa anataka amtumie kama daraja, bila hivyo kuwa na beef vitu vinawezekana kwani Ali Kiba ni msanii mkali na Dimaond ni msanii mkali kila mmoja ana fanbase kubwa tu kwa hiyo wanaweza kufanya muziki bila beef au laaah!! ziwe stunt tu za kibiashara sio mbaya!!
Tweet ya Davido aliandika “Pull half my crowd before you talk shit!! Looser
Na hii ni tweet ya Wizkid:-