Kama ilivyo kwa wasanii wengine wakubwa Marekani Ulaya na hata Afrika kwa sasa kuwa na vipindi vinavyoonyesha uhalisia wa maisha yao kama Kim kardashin, Kimora Lee Simon, Kendra, Na wengine, huku afrika nasi tumekuwa tukifata nyayo hizo kwa vipindi kama hivyo kuonekana kama kile cha Muigizaji maarufu wa nchini naijeria Omotola Jalade “THE REAL OMO SEXY”
kwa Tanzania napo sio jambo jipya sana kwa Msanii Wema kutokana na msanii mwingine mkubwa Lady Jay Dee kuwa na kipindi chake kama hicho Kinachorushwa kupitia Eatv “DIARY YA LADY JAY DEE’
Wema Sepetu alitangaza kwamba anaandaa reality show yake chini ya kampuni anayoimiliki “Endless Fame”. Muda umefika wa kuanza kuonyesha hiyo show yenyewe na Wema ameshatoa teaser au kionjo cha reality show hiyo ambayo inaonyesha baadhi ya vitu vinavyohusika kwenye show hiyo. Kwenye hii teaser inamuonyesha Wema anazungumzia kazi, mahusiano na katajwa Diamond humo,ziara za Wema na maisha ya nyumbani.
Viopindi kama hivi vina nafasi kubwa kwa jamii husika kutokana na kiu ya mashabiki wa watu wa aina hii kutaka kujua namna wasanii hawa wanavyoishi maisha yao baada ya kazi, pia inawaongezea kipato wasanii kutokana na kuuza vipindi hivi katika vituo mbali mbali vya luninga , kwa Tanzania mara hii tunanafasi kubwa zaidi kutokana na kituo cha DSTV kutoa nafasi kupitia Channel yake no 158 AFRICA MAGIC SWAHILI Kurusha vipindi vya aina hii
Kwa bahati niliwahi kukutana na Wema sehemu mbali mbali akiwa na crew iliokua inamchukua kila alichokua anafanya nikidhani ni movie lakini leo nimepata majibu kamili
Pongezi nyingi kwa wema na naamini katika hili ni hatua nyingine ya kumtoa zaidi mwanadada huyu