Dj Khaled kwa kushirikiana na Heads Audio na Olufsen kutengeneza headphones zinazoitwa “we the best”, Kama ilivyo kwa Dr. Dre kabla hajauza headphons zake zilizokuwa chini ya Dr Dre Beats Electronics Company na baadae kuziuza kwa kwa kampuni ya Apple dola bilioni 3 mwezi uliopita na kumfanya kuwa msanii anayeongoza kwa mkwanja duniani.
Hardworking pays Dj Khaled na baada ya kuhustle kusaka mkwanja nae amezindua headphones zake zinazoitwa “We The Best”.
“Leo nafuraha sana kutangaza kwamba nimeshirikiana na Heads Audio na Bang Olufsen kutengeneza We the best sound na kuingiza sokoni, We the best inawakilisha muziki mzuri katika burudani, nikiwa na Bang Olufsen band, wasikilizaji wamepata kifaa chenye ubora cha kusikilizia muziki tutaendelea kuchukua utamaduni wa ubora uliopo ndani ya Bang Olufsen na itawapa wasikilizaji kusikia muziki vile vile kama navyokuwa nikitengeza wakati natengenez ngoma studio”. Alisema Dj Khaled.
“ Nahisi fresh sana kutengeneza kitu kinachoendana na muda na muhimu zaidi ni jinsi ubora wake ulivyo katika kutengeneza muziki mzuri katika sayari tuliyopo sasa. Ungana na na mimi katika safari hii ya we the best sound, hakika hautudhika, We the best, the brand you can trust H6 Dj Khaled by B&O” Alisema Dj Khaled.
Kati ya wasanii wengine wa hip hop wenye headphones ni 50 cent na Ludacriss