Maisha ni njia iliyojawa na vikwazo na changamoto nyingi , lakini kama haupo imara unaweza ukaanguka, ni kama Sunami ilivyopiga na kulaza miti na majani yote yaliyokuwa ufukweni mwa bahari lakini baada ya siku chache mbele vitu vyote vilisimama.Hivyo ndivyo na sisi binadamu tunavyotakiwa tuwe kwa sababu hakuna mtu atakayekuja na kukubeba bila wewe mwenyewe kujituma, kutumia akili yako na nguvu zako ili kuleta mabadiliko katika maisha yako na jamii nzima.
Hii ni sawa na maisha tunayoishi kila siku, unakutana na magumu mengi muda mwingine magumu hayo yanakudhohofisha kabisa kwa kiwango ambacho unaona kama unaonewa, unaweza ukajiuliza hata kwanini unaishi. Lakini kila anayeishi Mungu anakusudi juu yake ndo maana yuko hai, amini kile kilicho kichwani kwako, kile unachokiota kila kukicha na kukifanyia kazi “Dream worth than money” huwezi kupata pesa bila kuwa na ndoto.
Utakutana na watu wengine watakutia moyo katika kile unachokifanya na wengine watakukatisha tama, lakini wewe kama unapenda unachokifanya endelea kufanya unachokiamini kwa sababu kama Mungu ameandika utafanikiwa hakuna binadamu anayeweza kuzuia. Narudia tena maisha ni njia iliyojaa vikwazo, na changamoto nyingi usikubali vikufanye uone kama hauoni mbele pigana.
Baada kushinda tuzo ya matangazaji wa redio anayependwa na kipindi cha redio kinachopndwa katika tuzo za watu, Millard Ayo alikuwa na haya ya kusema kupitia twitter:
“Kuna kitu watu wengi hawajui kuhusu kazi yangu, my bro Godwin Gondwe ndio mtu wa kwanza kunilipa pesa nyingi toka nimeanza utangazaji, nilikuwa nafanya kazi kenye redio ya dini na mshahara wangu ulikuwa elfu 20 kwa mwezi, elfu 5 kwa wiki, Gondwe alinifuata na kunipa dili. 2006 Gondwe alinipa kazi ya tangazo la redio kwa malipo ya laki 2, ndio ilikuwa mara kwanza nashika pesa nyingi kwenye maisha yangu.
Ni pesa ambayo pamoja na kuifanyia mambo mengine, nilinunua taa ya kuchaji maana nyumba niliyokuwa naishi Keko Machungwa haikuwa na umeme. Najua nina watu wengi wanapitia magumu kuliko mimi, tusivunjike moyo watu wangu! Hatujui ukurasa wa mbele tumeandikiwa nini. Baada ya kukosa kazi kwenye vituo vitano vya redio Dsm, Wapo redio walikubali kunipa nafasi ya kazi kwa makubaliano hawatonilipa.
Nilikubali baada ya kujua nilichokua nahitaji sio pesa bali ni CV! Ndio hapo nikawa natumia pesa yangu kutafuta habari na kuzipeleka ofisini. Mzee wangu ambae alikuwa dereva wakati huo aliniamabia hiyo kazi wasiyokulipa vizuru, ukiifanya vizuri HAWATOKUACHA mwanangu! Weka nguvu yote. Na kweli nilifuata yam zee, nikawa nakuja ofisini J3 hadi Jumamosi, wenzangu wengine watatu wasiolipwa waliacha kazi.
Japokuwa nilikuwa na ndoto za kuingia studio kutangaza, niliambiwa hakuna hiyo nafasi bali nitakuwa ripota tu kwenda kuchukua habari mtaani. Ila kwa ari niliyokuwa nayo wiki tatu baada ya kuanza kazi bosi alianza kunilipa elfu 5 kila Ijumaa yani elfu 20 kwa mwezi. Najua watu wengi wanataka kazi hela mbele ila kwenye huu ulimwengu wa nafasi 5 za kazi wanaojitokeza elfu 1, inabidi tufikirie tena.
Hkuna ubaya kuanza kazi hata kwa kujitolea inapobidi, nafikiria kama ningekataa kujitolea baada ya kukosa kazi kotr huko ningekuwa wapi? Miakamitatu ya Wapo redio, mwaka wa kwanza nililipwa elfu 5 kwa wiki, wa pili elfu 10, wa 3 elfu 25 sababu kiukweli sio redio ya biashara.
Nilishinda tuzo yangu ya kwanza ya utangazaji #TanzaniaRadioAwards nikiwa na mshahara wa elfu 60 kwa mwezi. Joseph Msami aliekuwa TBC1 na apo Redio aliamua kuniombea kwa boss ili nianze kuingia studio kutangaza, hii ni BAADA YA KUNIONA naripoti. Kila nilipokwenda kutafuta habari DSM nilikuwa nalipa daladala kama Mwanafunzi kutumia kitambulisho cha Mbezi Beach High School mpaka 2006.
Nauli na pesa ya kula mchana nilikuwa natumiwa na mama yangu ambae ni mwalimu Arusha lafu nakwenda kuipokea pale Scandnavia pale Kamata Dsm. Nilianza kazi na miaka 18 TVZ Zanzibar ambako sikuwahi kulipwa hata posho lakini wao wa Wapo Radio wamenitengenezea nilicho nacho leo.
Kwa sababu hakuna utaratibu wa kuwa na msaidizi, hicho ndicho kilichonijenga na kunipa utaalamu kuweza kufanya kila kitu mwenyewe, hawakunipa pesa lakini walinipa MAISHA NINAYOISHI sasa hivi! Uzoefu na ujuzi nilioupata kwao ndio ulinisaidia kupata kazi ITV/RadioOne. Kuna mambo yangu makubwa manne sijawahi kuyazungumza popote ila naamini siku moja nitapata nafasi ya kuyazungumza tu watu wangu.
Wakati mwingine tunafanya vitu ambavyo hatuvipendi maishani bali”tumevitaka tu” mfano mimi nilikuwa Fundi wa TV, Radio na Sattelite dish. Nilitamani hiyo kazi sababu niliona imewalipa Wajomba zangu lakini kumbe Mungu hakunipangia huko na sikufanikiwa kabisa hivyo nikaacha. Hapo pia ndio nikajifunza sio kila kinachomfanikisha mwenzako kitakufanikisha na wee, yani tunatakiwa kufanya vile tunavyoviamini ni vyetu.
Ni lazima niwashukuru tu watu wangu wa nguvu wote yani! Hii love mnayonionyesha mpaka mitaani ni KUBWA SANA na ndio inanipa nguvu kiukweli. Nashukuru baba yangu ambae alikua mkali sana lakini akaniruhusu kushiriki utangazaji kipindi cha watoto Clouds FM Arusha nikiwa na miak 13. Namshukuru sana kaka yangu Gardner G Habash, alinisaidia SANA kutafuta kazi Clouds FM mwaka 2007/2008 japo sikupata, nikapata ITV/RadioOne.
Ukweli mwingine wa moyoni, lazima NIWASHUKURU Clouds FM, maisha yangu wameyabadilisha kwa kiasi KIKUBWA SANA yani, nitaeleza tu siku moja”.
“Dream Worth Than Money” Millard Ayo Hakukata Tamaa
Previous Story
Dj Khaled Azindua Headphones Za "We The Best"
Related Posts
-
-
Salmamsangi.com Inawatakia Eid El-Fitr Njema Yenye Amani Na Utulivu Mkubwa
-
Haya Ndio Makosa Yanayoharibia Watu Wengi maisha Katika kipindi Cha Umri Wa Miaka 20
-
HONGERA HELLEN
-
Gonga White Beach Party Photos From Mobil
-
Picha: Tazama Harusi Ya Muandishi, Muandaaji Na Matangazaji Wa Dawati La Michezo Channel Ten Na Magic Fm Baraka Ngemba
-
Video: Alichokisema Floyd Mayweather’s Baada ya Kumpiga Canelo Alvare