
Katika kuelezea experience yake katika tour iliyomalizika akiwa na mwanadada Rihanna, Eminem pia ametaja filamu zake anazozipenda ikiwemo “Step Brothers”.
Hivi karibuni amemaliza tour iliyokuwa ikiitwa The Monster Tour, amesema ilikuwa rah asana kufanya tour akiwa na Pop star Rihanna.
“Ni fresh sana, Ilikuwa raha, ilikuwa wakati mzuri, Mimi ni mtu wa watu, Sana mimi ni mtu wa watu” alisema Eminem akipiga stories na Shade 45.
Alipoulizwa jinsi alivyopanga nyimbo zake, Eminem alisema kila wakati anafanya mabadiliko kwenye nyimbo anazoperform
“Kila wakati tunajaribu kutengeneza list ambayo inaendana na mahali na wakati, Kama ni kurudia za zamani au kucheza mpya, hatujawahi kufanya kitu kile kile sehemu nyingine” aliongeza Eminem.
Nje ya kuongelea kuhusu tour hiyo, aliongelea msimu unaokuja wa NFL na timu yake anayoipenda Detroit Lions.
“Sisemi Lions watafanya vizuri au vibaya, sitaki kutabiri, The Lions kila wakati timu yangu, Itakuwa fresh sana kuona kumuona kocha Jim Caldwell akifanya vitu fresh na jinsi kila mtu akifanya nae kazi, itakuwa poa kwa sababu tunao watu wenye vipaji sana” alisema Eminem.
Eminem pia alitaja Pittsburgh Steelers, San Francisco 49ers na Dallas Cowboys kuwa ni timu ambazo pia anazisupport.
“Step Brothers ni moja kati ya movies anazozipenda, nyingine ni Superbad na Knocked Up”
