Klabu ya Manchester United imetangaza kuwa Kocha na Meneja wake Sir Alex Ferguson atastaafu rasmi, na hii itakuwa ni May 19 baada ya mechi ya timu yake dhidi ya West Bromwich Albion.
Katika kuangaza maamuzi yake haya Ferguson amesema kuwa amelifikiria swala hili kwa uzito wake wote na amena kuwa ni wakati muafaka kufanya hivyo.
Fergie amesema kuwa, ilikuwa ni muhimu kwake kuhakikisha kuwa anaiacha timu hiyo ikiwa juu kabisa na katika hali nzuri na anaamini kuwa amelifanikisha hilo.