Andy Murray anajiandaa kujitoa mapema kwenye mashindano ya Australia Open kukiwa na umuhimu wa kufanya hivyo ili aende akawepo wakati mke wake akijifungua mtoto wao wa kwanza, Akiwa ni bingwa namba 2 wa Tennis duniani ambae amekuwa akipoteza katika fainali katika michezo minne ndani ya Melbourne, ameweka wazi atajitoa katika shindano kama mke wake Kim atakwenda kujifungua mapema. Mashindano ya Australia Open yanaanza tarehe 18 – 31 mwezi Januari na mtoto wa Andy Murray anategemea kuzaliwa Februari.
Murray hivi karibuni aliongoza Great Britain kwenye Davis Cup,pia alisema kwamba uamuzi wa kumaliza mazoezi yake ya awali mapema katika kambi ya Dubai ilisababishwa na hali nzuri ya usafiri kurudi UK.
“Nilikuwa pia niende Dubai au Miami lakini wazi kabisa Kim mimba imekuwa kubwa sana, ni rahisi kurudi kutoka hapa,ndege zote zinaondoka jioni kutoka Miami,ambapo hapa unaweza ukaruka muda wowote katika siku” amesema Andy Murray.
Bingwa huyo namba 1 Uingereza atarudi kwenye fukwe za nyumbani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za BBC Sports Personality of the Year Jumapili huko Belfast.