
Kutoka lebo ya Fishcrab, Management ambayo ilikuwa inamsimamia Mr Nice baada ya kurudi katika game hivi karibuni ambapo msanii huyu alikuwa chini ya Lamar, limetoka neno hasa baada ya msanii kuingia rasmi na kuanza kazi na lebo ya Grandpa ya huko kenya wakati ambapo wengi walikuwa wanafahamu juu ya mkataba wake na Fishcrab ambao ndio ulikuwa bado mpya mpya.
Kwa Masharti ya kutokutajwa jina lake moja ya msemaji kutoka Management ya Fishcrab, amesema haya kuhusiana na tabia, na mwenendo wa Mr Nice katika dakika za mwisho kabla hajabadilisha code za eneo ambalo ameamua kwenda kuendeleza kazi zake.
Msemaji huyo amesema kuwa Mr Nice alianza utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kuja kwenye show akiwa amelewa aua asitokee kabisa na wakati mwingine kutotekeleza yale anayoagizwa Mabos zake, hata kufikia kuamua kumsimamisha kwa kipindi fulani ili atakapokuwa tayari na serious aseme na kazi ziendelee.
kwa mujibu wa msemaji huyo ni kwamba bado wana mkataba na Mr Nice ambao ni wa miaka mitano na kwamba ni mkataba wa kisheria kabisa uliosainiwa mbele ya mwanasheria na kwamba hata kopi yake ya passport yake ipo huko.
Hata hivyo Inavyooneka ni kwamba Mr.Nice alihamia Kenya na kusain mkataba na GrandPa bila kuwafahamisha Fish Crub
Mr. Nice amekua aki make headline katika vichwa via habari huko kenya tangu asaini mkataba na grandPa hata kufanyiwa mahojiano na Kituo kikubwa cha televisheni Nchini Kenya The Citizen.
unaweza kuona mahojiano hayo pia.
