Floyd Mayweather Jr ni mwanamasumbwi asiyepigika kirahisi na pia anaongoza list ya wanamichezo wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi duniani, pia anashikilia namba 7 katika list ya mastaa wenye ushawishi duniani. Nani staa gani anayeongoza list hiyo?
“Nataka niwashukuru Forbes na pia kuwavulia kofia kila mmoja katika list hii, Nafurahia kwa kila aliyepo katika list hii, nafuraha sana kwamba na bahati kuwa namba 7,” Aliandika Flloyd na picha ya top 10 ya mastaa wenye ushawishi duni.
Beyonce anaongoza akiwa kileleni kufuatia mwaka wake kuwa mzuri na tour kali kabisa, Taarifa kutoka Pollstar zinasema kwamba Beyonce alifanya show 95 na alitengeneza mkwanja dola milioni 2.4 kwa show moja na pia alitoa albamu aliyoiita jina lake Beyonce ikiwa ni ya video.
Ngoma ya Drunk in Love imeuza zaidi ya copy milioni 1 na kufikia kiwango cha platinum, Bey aliungana na mume wake Jay Z kwa ajili ya tour yao ya kwanza kama mume na mke. Ukiacha muziki Queen Beyonce anaingiza millions kwa kushirikiana na makampuni kwa kutangaza bidhaa kama Pepsi na H&M.
Pia ana kampuni ya nguo inayoitwa House of Dereon, pia anazo perfumes pilse, heat na rise.Ukirudi kwa Floyd Mayweather Jr. yeye anashikilia namba 7 katika list hiyo.
Yeye ni mwanamichezo anayelipwa zaidi kutokana na Forbes , mwaka mmoja uliopita Mayweather aliingiza dola milioni 105 katika pambano lake dhidi ya Marcos Maidana na Canelo Alvarez.
Celebrities:Hi indo list nzima ya mastaa 10 wenye mkwanja.
1. Beyonce
2. LeBron James
3. Dr. Dre
4. Oprah Winfrey
5. Ellen DeGeneres
6. Jay-Z
7. Floyd Mayweather Jr.
8. Rihanna
9. Katy Perry
10. Robert Downey Jr.