Future na Ciara hawakukaa kwa muda mrefu baada ya kutengana, kwa sababu Ciara yuko imara kuhusu mtoto wake na anahitaji baba yake awe karibu na mtoto wake saa 24 na siku saa 7 za wiki.
Chanzo kimoja karibu na Future ameiambia TMZ, kwamba Future na Ciara wanaishi pamoja tena na wanajaribu kurekebisha mambo yaende vizuri waendelee na mahusiano yao fresh.
Future anaweza kusaidia kumlea mtoto wao wa miezi minne anayeitwa Future Zahir.
Ciara lazima atataka kutazama ya nyuma, kwani ndiye aliyekuwa akisema kwamba Future alikuwa na michepuko wakati akiwa kwenye tour na kuvunja mahusiano yao mwezi uliopita.
Taarifa zinaeleza Ciara hakuvutiwa sana kushirikiana katika kumlea mtoto wao, lakini anasema anaamini kwamba Future na baba mzuri na hilo ni swala zuri kwa mtoto wao kama baba atakuwepo wakati malezi.
Vizuri sana Ciara hajawa mbinafsi, kama anaamini kwamba Future ndiye aliyemdanganya, lakini kwa sababu ya mtoto fresh tu wawe pamoja.