Game ameshtakiwa na kampuni ya promosheni inayopatikana Lousville Kentucky. Taarifa zinasema kwamba kesi imefunguliwa na Dream Team Entertainment LLC wiki iliyopita, repa Game aliacha kufanya show ya tamasha la kati kati ya mwaka la Kentucky Derby mapema mwaka huu kwa sababu hakuwa kama marepa waliokuwa katika headline. Taarifa za mahakama zinasema kwamba repa huyo huyo alishasaini mkataba kwa ajili ya tamsaha hilo Aprili 11 mwaka huu na alipewa dola 35,000 ikiwa ni Advance kwa ajili ya kufanya show hiyo, ambayo ilifanyika Mei 2 huko Louisville Kentucky. Katika shauri hilo Dream Team Entertainment LLC wamesema walipokea simu kutoka kw amtu ambae anamuwakilisha Game akisema kwamba Game hataperform katika tamasha hilo bila yeye kuwa kati ya wasanii wanashika headline kwamba wataperform katika tamasha hilo. Promota anasema kwamba Game mara akaacha kutokea kuperform kwenye show hiyo na
hakurudisha dola 35,000 au alipe dola 30,000 za ada ya kuhairisha show. Kutokana na usumbufu uliojitokeza Dream Team Entertainment LLC inatarijia kulipwa dola 75,000 kulipia hasara iliyojitokeza. Mwaka 2012 40 Glocc alifungua kesi dhdi ya Game wakidai dola milioni 4.5 kufuatia shambulio lilitokea mapema mwaka huo, 40 Glocc alisema alishambuliwa na Game na watu wengine 15 nje ya jengo hilo huko Hollywood California.