
Sulley Muntari na Kevin Prince Boateng wamefukuzwa kwenye kikosi cha timu ya Ghana kwa utomvu wa nidhamu.
Taarifa kupitia mtandao wa Chama cha mpira nchini Ghana kimesema wachezaji hao wamefukuzwa.
Iliongeza kwamba Boateng alitumia lugha chafu akimlenga kocha wa timu hiyo Kwesi Appiah na mtandao ulisema Muntari yeye walishikana na kiongozi wa juu wa kamati kuu.
Taarifa zimekuja saa chache kabla ya mechi ya Ghana dhidi ya Portugal leo Alhamisi, Timu hiyo ya Ghana bado inanafasi ya kuweza kusonga mbele.
