Dakta Sengodo Mvungi enzi za uhai wake Akiwa hospitali
Habari ni zilizopo ni kwamba punde zinasema kwamba Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dakta Sengodo Mvungi(Pichani) amefariki katika hospitali ya MillPark huko Afrika ya kusini alikokuwa akipata matibabu.
Dk Mvungi alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Oktoba 2 Mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.
Mauti yamemkuta Mnamo Majira ya Saa Tisa na Nusu.Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.
MOblog inatoa pole kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Familia, Chama cha NCCR na Watanzania wote kwa ujumla. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.