Hospitali ya Kairuki imesema inajiandaa kujenga kituo cha kisasa kwa ajili ya kutoa huduma kwa kina mama zikiwamo za wanawake wasiopata mimba na hivyo kuwazalisha kwa kutumia chupa.
Hatua hiyo ni sehemu ya mipango ya baadaye itakayotelekezwa na hospitali hiyo ambayo kesho itaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake na muasisi wake, Marehemu Profesa Hubert kairuki mwaka 1987.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Asser Mchomvu, alisema kuwa mbali na ujenzi wa kituo hicho, hospitali yake itanunua mashine ya kisasa ya uchunguzi T Scan, kufungua matawi ya hospitali hiyo mikoani, kusitisha upasuaji wa kutumia visu, kutoa elimu kwa umma na kuendelea kushirikiana na serikali katika sekta ya afya.Dk. Mchomvu lisema kuwa hospitali hiyo imetoa huduma mbalimbali za bure za kusaidia jamii kama sehemu za madhimisho hayo kama utoaji wa tiba ya bure, dawa, madawati na vifaa vya tiba iliyogharimu Sh. milioni 12.
Alisema kuwa licha ya changamoto mbalimbali walizokutana nazo, hospitali hiyo imefanikiwa kuanzisha chuo kikuu cha kwanza binafsi nchini.
Aidha, imefanikiwa kubuni na kuanzisha mfumo wa kumbukumbu za wagonjwa unaotumia mtandao wa kompyuta badala ya kutumia kuhifadhi kumbukumbu hizo kwa kutumia mafaili.
Kwa mujibu wa Dk. Mchome, hospitali ya Kairuki imetoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 4,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Kuhusu Chuo Kikuu cha Kairuki, Dk. Mchome alisema tangu mwaka 1998, limeshazalisha wahitimu 971.Akizungumzia ujenzi wa kituo cha wanawake, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Dk. Clementina Kairuki-Mfuka, alisema ujenzi huo wa jengo la ghorofa sita utaanza baada ya kukamilikataratibu zote na kwamba utagharimu Sh. bilioni 7.2.Dk. Clementina ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, alisema jengo hilo litakuwa na kuduma mbalimbali kama maegesho ya magari, sehemu ya dawa, maabara, vyumba vya kulaza wagonjwa na ofisi za madaktari. Vile vile pembeni utajengwa uwanja mdogo wa helikopta.