Kwanza nichkue Fursa hii kumshukuru Mw/Mungu (S.W) Kwa kiniwezesha kuishi hapa duniani kwa Miaka 29 sasa nikiwa na afya njema, Amani, Furaha, Familia, Ndoa, kazi , Marafiki na kila burudani ya kunifanya nifurahie maisha.
Kwa kweli nitakuwa ni mwenye nidhamu ndogo kama nitamlalamikia Mw/Mungu kwa lolote lile, kwani mimi naweza sema nimekuwa ni shuhuda mzuri kwa Mungu wangu kwa kweli amekuwa akinijalia kila nililomuomba tena kwa wakati muafaka kabisa na amenifanya nione furaha raha na amani ya kuishi katika kipindi changu chote cha miaka 29 Sasa hapa duniani nasema Ahsante sana mungu kwani ukimtumainia yeye hakika hakuna kinachoshindikana chini ya jua Amini lakini amini kwa asilimia 100.
Mama yangu
Mama Yangu na MAma yangu mkubwa: Wamekuwa ni mwongozo mzuri wa maisha yangu katika kipindi chote hiki nilichofanikiwa kupumua kwa salama hapa duniani, bado nakumbuka mafundisho yake mengi kipindi nipo mdogo naishi kwa mfano wao na ndio maana nasonga salama, nawapenda sana na nazidi kuwaombea maisha marefu hapa Duniani.
nikiwa na mume wangu Mziray Abbas
Mume wangu: hapa ndipo huwa maneno huniisha, Maneno hayatoshi kwa kumuelezea mwanaume huyu aliyeingia katika maisha yangu na kunifanya nisahau kama kuna shida hapa Duniani katika kipindi cha miaka tisa ya kuwa pamoja kuanzia uchumba hadi ndoa kwakweli mume wangu ni kati ya wanaume wachache sana duniani wanaotambua wajibu wao kwa wake zao…. Nitake nini mie kwa huyu baba jamani looo sina zaidi ya kumuombe kwa Mw/Mungu amjaaliye maisha marefu na ya amani.
Ndugu Zangu wamekuwa ni watu wangu wa karibu kunisaidia kunisapoti katika kila hali ilimradi waone natimiza ndoto zangu, Heshima wanaonipa ndugu zangu wananifanya nijisikie mbora miongobi mwa wabora Alhamdullilah
Wafanya kazi wenzangu wote wa Africa Media Group kampuni ninayofanyia kazi, jamani hakuna tena familia kama ile, wamekuwa ni watu ambao wananifanya maisha niyaone mepesi wakati wote, wamenikuza na kunifundisha kuishi na watu kwa vitendo tangu utoto wangu mpaka utuuzima huu nasema utoto kwasababu kampuni yangu ndio kampuni ya kwanza mimi kufanyia kazi tangu nimetoka shule nikiwa na umri wa miaka 18 tu leo nina miaka 29 ni sawa na nyumbani kwangu kwakweli nawapenda sana na InshaAllah Mw/Mungu aendelee kutujaalia mshikamano na mapenzi tele tuendelee kusogeza hili gurudumu la maisha mbele.
wapo watu wengi wa muhimu nyuma ya pazia ambao wameweza kunifanikisha mimi kufika hapa nilipo leo nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa nikiwa na amani matumaini na furaha tele Nao nasema Ahsante na InShaaLah sina cha kuwalipa zaidi ya Dua nyema kwa Mwenyezi.
Watu wengi wamekuwa hawaamini mara niwaambiapo umri wangu, wakidhani mimi ni mdogo kuliko umri niliona, labda ni kutokana na monekano nilio nao wa mwili mwembamba sura ya utoto nk. wengi wamekuwa wakiniuliza nini nafanya kuendelea kubaki kuwa nilivyo katika kipindi chote ambacho wamekuwa wakinifahamu, Labda tu niwaambie jamani
Nadhani mimi ni mti mkavu ule wengi wanauzungumzia nimegoma kunenepa hata nile nini, sio kama naupenda wembamba sana lakini ni lazima nijikubali kwasababu ndio majaaliwa yangu, wengi wanadhani najinyima kula kwasababu bado nataka kuonekana kuwa mrembo miss kawa wenyewe wanavosema si mbaya kama ni hivyo mwanamke wake urembo lakini sivyo mfikiriavo mimi nakula kila kitu kwa kiasi ninachojaaliwa kula bila kujihini watu wa karibu yangu wanajua hata wengine wamekuwa wakinisakama kwa maneno kwanini nakula sana lakini sinenepi kiukweli sina majibu ya kuwapa kwasababu hata mimi sijui ni kwanini.
Kuhusu Sura jamani kwanza niwaambie namshukuru mungu kwa kuniumba jinsi nilivyo najua uzuri wa mtu u machoni mwa mtazamaji hapa nawajibu wale wenyekuwa wakiniuliza maswali mengi kuhusu nini natumia kwanini nipo hivi nk kama haikuhusu pita tu hapa wala usijiharibu sura yako kwa kunyali
Kwanza uso wangu haujui kemikali za iana zozote tangu nakuwa na akili mpaka sasa sikuwahi kushawishika kwa cream wala mkorogo maana kama ni rangi alonipa mungu ilinitosha Alhamdullilah, namshukuru mama yangu alinisihi sana nisije nikajiharibu maana aliamini mimi nipo sawa tu kama mungu alivoniumba nilimuelewa nashkuru. lakini pia mimi jamani sinaga uda wa kukasirika, kuweka jambo rohoni, sijajaaliwa roho mbaya mimi wala kumchukia mtu nadhani hayo ndo mambo yanazeesha wanawake wengi sana kifikra mpaka kimwili, Mimi sina muda wa kulea tatizo limejitokeza na deal nalo nimemaliza ni vizuri kukabiliana na cvhangamoto badala ya kusononeka kulalamika na kuikimbia weka wazi kuwa huru. mimi ni mkweli sana na ndio maana watu wengine wameshindwa kunielewa ila penye ukweli tutamaliza sina sababu ya kudanganya kwa kifupi i live free… nimechagua kuwa na furaha naishi maisha yangu kwa namna yeyote maisha ya mtu na mamo yake hayanihusu naridhika pale paliponitosha na nasema Alhamdullilah
Hizi ndi lotion nimekuwa nikitumia kwa ajili ya mwili wangu wote kuanzia usoni mpaka miguuni kwa kipindi chote tangu nina akili zangu tiamu nikikosa sana nitapaka mafuta ya mgando vaseline.
Siri nyingine Wasichana acheni kutumika sana na wanaume, wanaume wanatufanya tuchoke haraka sana, usitumike kwasababu ya pesa wakati unapita na utabaki tambara wanaume wanatupenda wakitoana freshh baada ya kututumia na kutuchakaza wanatutupa chagua wako mmoja tulia nae mfanye maisha pesa ipo hata bila kutumika kimwili tuache uvuvu na jia za mkato tujitume tutakuwa hutu na hakuna atakayetuendesha.
Kula vuzuri, maji mengi, juice tupate muda wakulala tupunguze starehe na pombe sigara bangi na kila aina ya mihadarati vinatuchosha tunazeeka haraka msichana anamiaka 20 anaonekana kama anamiaka 40 ukiuliza starehe jumatatu kwa juma tatu sio sifa mnaisha.
Jikubali, Jitambue, Jiamini,Jipende na jipendezeshe, jivunie kuwa wewe kwa maana hakuna Binadamu mwingine kama wewe hapa Duniani ishi maisha yako weka malengo fuata ndoto zako na zitimize.
Stay True, Stay Real because your you and i’m me.
ZAIDI YA UNIJUAVYO:
NIMEZALIWA 24/07/1984, MTOTO WA KWANZA KATIKA WATOTO WAWILI WA BI SHUFAA MSANGI, NIMESOMA HADI ELIMU YA SEKONDARI,NIMEKULIA UPANDE WA MAMA YANGU, NIMEKUTANA NA BABA YANGU NIKIWA NA MIAKA 19, NIMEANZA KAZI NIKIWA NA MIAKA 18, NIMEFANYA KAZI SEHEMU MOJA KWA KIPINDI CHA MIAKA TISA BILA KUSHAWISHIKA KWENDA SEHEMU NYINGINE, NILIPOANZIA AJIRA YANGU YA KWANZA NDIPO NILIPO MPAKA LEO, CHANNEL TEN NA MAGIC FM, MME WANGU NI KABILA LANGU, SINA MTOTO, NINA MIAKA MITANO KWENYE NDOA LAKINI UHUSIANO WA MIAKA TISA NAMME WANGU TANGU TUKUTANE, NAOGOPA GIZA, SIWEZI KULALA MWENYEWE, SISINZII MPAKA NIAMUE KULALA, SINA CHUKI, NAMPENDA MDOGO WANGU KULIKO KITU CHOCHOTE HAPA DUNIANI. BABA YANGU NI KRISTO THEHEBU LA SABATO LAKINI MIMI NI MUUMINI WA DINI YA KIISLAMU, UKOO WA MSANGI NI UKOO WA UPANDE WA MAMA UPANDE WA BABA MIMI NI UKOO WA TENGA.
Ukweli Nimeshtuka sana kuona nimetimiza miaka 29 ,Mama yangu? umri unakwenda na sasa nimekua mtu mzima kabisa OMG lol, kama mchezo vile 30 hii hapa duuuu fainali uzeeni mwe inabidi niwe serious sasa hahahahh….
kwaheri utoto karibu ubibi.
Happy Birthday To me.
6 Comments
Happy birthday Salma.live long mama u real inspire me.
Happy Birthday Salma Msangi. Be safe and take care.
ahsante sana Fatma na Irene thank you dols
happy birthday mamy muombe mungu aendelee kukupa afya njema maana maradhi noma.
AMEEN INSHAALAH manka
uwiii nimeipenda hii article.live longer dear.namungu akujalie watoto wengiii sana no wawili hahaha.nimekupenda