
Madaktari walishangazwa pale mwanamke mmoja wa Colombia alipokimbizwa hospitali baada ya kuwa anasumbuliwa na maumivu ya tumbo, ndipo walipogundua mizizi ya kiazi inaota kwenye uke wa mwanamke huyo. Mhuguzi aliyekuwepo hospitalini hapo anayeitwa Carolina Rojas alidhani ni utani pale alipoona mizizi ikikua kutoka kwenye uke wa mwanamke huyo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alionekana kushtushwa sana na tukio hilo alisema mama yake alimwambia aweke kiazi kama dawa ya kumfanya asipate mimba (contraception) na kilikaa kwa wiki 2 kwenye tumbo lake la uzazi. Aliambia HBS News mama yake alimwambia kwamba kama akitaka asipate mimba anatakiwa aweke kiazi sehemu ya uke wake na alimuamini mama yake. Ni bahati yake kwa sababu matibabu yake yajamgharimu maisha yake ametibiwa na pia haikuhitaji upasuaji wowote.
