
Wakati tunaringishia Vidole vyetu na vipete vya Tanzanite vya Gram mbili mbili wakati wa kuombwa uchumba sijui Lola Natasha Mchumba Wa Peter okoye kutoka kundi la Psquare yeye afanyaje hahahaha… nimekomaaaaaaaaaaaa
Katika kuonyesha kuwa Wanamuziki hawa wamefanikiwa jana kupitia Ukurasa wake wa instagram Peter alitupia Picha ya zawadi ya Gari aina ya Range rover kwa ajili ya mpenzi wake Lola ambaye alikua akimtaka uchumba Rasmi
Habari ilikuwa hivi, sasa siimagine hilo lipete hapo ni maalmasi ya kina diamond ya mahela mangapi mwe….
Unakataajeee sasa hapo? lol.
Unahaki ya kudolishia dada Lola, kitu kinaeleweka ha ha ha… Ringa mama Kupendwa ndio Huko, kupendwa kuthaminiwa….
Unakumbuka zawadi uliopewa wakati unaombwa uchumba? au uliubembelezea mpaka ukaamua kwenda kuinunua pete mwenyewee???
Tafakari.
