The Breakfast Club ni show maarufu sana nchini Marekani, kupitia show hii hii ndio sehemu beef ya Tyga, Kylie Jenner, Amber Rose pia ilisikika wote walienda kwenye show hii nakupiga stories.
Naye mkali wa ngoma ya “New Flame” Breezy ameenda kwenye show hiyo kwa ajili ya kuongea mawili matatu na mashabiki wake, ambapo aliongelea vitu kibao ikiwemo Tour yake na Trey Songz, mahusiano, ubaguzi wa rangi katika muziki, kufanya kazi na Tyga, Ugomvi wa ndani kwa ndani ya tuzo za Grammy, mawazo yake kuhusu muziki wa R&B na marepa pia mawazo yake kuhusu Drake.
Akimuongelea Drake alisema “ Yule mshikaji simuoni kama ni ishu, sikufanya nae ngoma, alikuwepo tu studio, alikuwa ni shabiki” alifunguka Chriss Brown.
Mtangazaji wa kipindi hicho anayeitwa Charlamagne Tha God alimuuliza Breezy kama alikuwa rafiki wa Drake, msanii huyo alijibu “Hapana, maongezi muda huo huo yakahamia kwa girlfriend wake zamani Rihanna na watu wengine maarufu waliotoka na Rihanna baada yake.
“Msichana mkubwa sasa, wa kwanza, nani tena ataenda kwake? Nani tena katika gemu hili ataenda kwake? Repa fulani muimbaji wa kizamani?
Baadae Brown alieleza ushindani katika gemu unaepelekea kuchukiana katika kiwanda cha muziki, kutokana na Chriss Brown, anasema kutokana na mambo kubadilika inakuwa ngumu kuwa na marafiki wa kweli na wasanii wengine.
Check Video ya mahojiano——–