
Picha ya Pamoja Ya Washindi Wa tuzo Za Watu
Tuzo zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu kubwa Tuzo za watu ziilizoandaliwa na mtandao wa Bongo 5 zilifanyika usiku wa Ijumaa 27 Juni katika hoteli ya Serena hoteli zikihusisha watu maarufu. Tuzo hizo zilihusisha vipengale mbali mbali kama ifuatavyo: Lady Jay Dee Commando alishinda tuzo ya video inayopendwa kwa video ya “Yahaya” kama kawaida , Na muimbaji wa kiume tuzo imekwendaa kwa Diamond na wimbo wa “My number one” , Mzee Majuto alishinda tuzo ya muigizaji anayependwa zaidi.
Lulu au Elizabeth Michael alishinda tuzo ya muigizaji wa kike anayependwa zaidi, tuzo ya mtangazaji anayependwa ilikwenda kwa Millard Ayo pamoja na redio show inayopendwa zaidi ilikwenda kwake tena Millard Ayo na kushinda tuzo mbili usiku mmoja. Mtangazajiwa BBC Swahili Salim Kikeke alishinda tuzo ya mtangazaji luninga anayependwa zaidi, Tuzo ya mwanamichezo anayependwa zaidi ilikwenda kwa Juma Kaseja, Muandaaji ya video anayependwa zaidi. Kwa mtangazaji wa kike anayependwa zaidi alishinda Salama Jabir na kipindi cha Mkasi.
Usiku huo pia ilizinduliwa video ya msanii wa Bongo flava Ben Pol ya wimbo “Unanichora” akiwa amemshirkisha Joh Makini video hiyo ilizinduliwa kama surprise na watu kuitazama katika big screen usiku huo. Watu mbali mbali wamewapongeza Bongo 5 kwa kuandaa tuzo hizo ikiwemo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Usiku huo pia ulihudhuriwa na mashabiki wengi na mwanasiasa aliyekuwepo ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, Na hizi ni picha mbali mbali za tuzo za watu usiku huo
Tazama Matukio Katika Picha
Mc Alikuwa Jimmy Kabwe
Mkurugenzi Mtendaji Wa Bongo 5 Lucas Akiwa Na Nancy Sumary
Meya Jerry Slaa
Millad Ayo Mshindi Wa Kipindi cha Radio Kinachopendwa Zaidi na Mtangazaji Wa Radio Anayependwa Zaidi
Salum Kikeke Mshindi Wa Mtangazaji Wa Televisheni Anayependwa Zaidi
Bab Tale Alipokea Tuzo Ya Diamond Katika Video Ya Muziki Inayopendwa Zaidi
Mzee Majuto Alishinda Muigizaji Wa Kiume Anayependwa Zaidi
Muigizaji Wa Kike Anayependwa Zaidi alikuw NI lulu
Jack Wolper Alitokea katika Filamu Iliyoshinda ambayo alicheza na marehemu kanumba
Mtangazaji Wa Kike Anayependwa Zaidi Ilikwenda Kwa Salama Jabir
Lady Jay Dee Alishinda Wimbo Uliopendwa zaidi ambao ni yahaya, Hapo muwakilishi akimpokelea tuzo kutoka kwa mbunifu Mustafa Hasanali
Maddam rita Akimtangaza mshindi
Mzee Kassongo Akimtangaza Mshindi
Meya Jerry Slaa Akimtangaza mshindi
Msanii Enika Akitoa Burudani
Msanii Wa vichekesho akitoa burudani
Ripota Wako Kutoka Eneo La Tukio
