Spika wa Bunge Anne Makinda amewaasa Wabunge kutumia Lugha ya Staha ambayo ni ya Kibunge wakati wa kuchangia mijadala Bungeni.
Mhe. Makinda amesema, kuendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na maudhi kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni kuendelea kuliondolea hadhi Bunge.Pamoja na hilo, wabunge wanatakiwa kujikita katika kuchangia hoja zenye kutataua matatizo ya wananchi ili kutimiza wajibu wa kila mbunge wa kuwa wakilisha wananchi.
Mhe. Makinda , amesema, fursa ya kila Mbunge kuchangia lazima ilenge kutatua matatizo ya wananchi na sio kutukanana na kusahahu jukumu lilomblele ya kila Mbunge. Katika Picha ni baadhi ya waheshimiwa Wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2013/14 Mjini Dodoma.