
Mshiriki wa Big Brother Africa iliyopita miaka ya nyuma, Huddah Monroe amepewa deal ya kutangaza nguo na kampuni inayofahamika kama Vazzi.
Vazzi ilizinduliwa mwaka 2010 kwa lengo la kutengeneza nguo zenye ubora, zikiwa ni za bei nafuu na za staili mbalimbali kwa ajili ya Wakenya na watu wengine duniani.
Mwanadada huyo mwenye kick kwenye mitandao amepata deal hiyo ya kutangaza nguo za kampuni hiyo ya Vazzi.
“Ameingia deal ya kushirikiana na Vazzi, deal ambayo ataonekana akipromoti na kuonyesha nguo za Vazzi nchini Kenya” alisema meneja wa Huddah Medrine Mueni.
“nguo hizo zitakuwepo tops, T-shirts, jezi, hoodies, vest na biashara nyingine, zitakuwa za ubora wa juu na bei nafuu kwa kila mtu anaweza kununua aliongeza meneja wa Huddah”
