Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Tanzania katika Jiji la Dar Es Salaam imefikia 34 kipindi hiki Kikosi Maalum Cha Uokozi kikiendelea na zoezi la kuondoa kifusi ili kuangalia kama kuna miili zaidi imenasa chini ya mabaki ya jengo lenye ghorofa 16.
Jengo la Ghorofa 16 lililoporomoka Jiji Dar Es Salaam nchini Tanzania limesababisha vifo vya watu 34 hadi sasa Kwa hisani ya Ikulu ya Tanzania Zoezi la kusaka miili ya watu walionaswa kwenye malundo ya vifusi limeendelea kwa siku tatu mfululizo usiku na mchana ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Saidi Mecky Sadick amethibitisha wameshapata miili ya watu 34.
Miili kumi imepatikana kuanzia siku ya jumapili hadi mapema asubuhi ya leo ambapo Kikosi hicho kikitumia zana mbalimbali kimeendelea kuhakikisha kinaondoa kifusi na kufika chini ambako kuna ghorofa tatu.