Huwa Nasikitika sana ninapokaa katika makundi ya wanaume au wanawake wanamzungumzia msichana Fulani Ambeye labda anatoa harufu kwa namna moja ama nyingine, Huwa Najiuliza Inakuwaje mpaka mtoto wa kike Anatoa harufu mbaya toka mwilini mwake?
Ninapozungumzia swala la Harufu mbaya ni pamoja na Kutoa Harufu Ya Kikwapa, Mdomo, Jasho, sehemu za siri au hata nywele na nguo za ndani? Msichana, Mtoto wakikwe, Mwanamke kwanini Utoe Harufu Mbaya?? kwanini???
Hakuna swala la ugojwa katika Tatizo la kutoa Harufu mbaya, Ugojwa ni ugojwa tu na unajulikana na mara nyingi maradhi haya huja baada ya uchafu uliopililiza, Nasikia watu wengi wakisema mara nyingine ni maradhi.
Hapana Ni uchafu kuto kujisafisha inavyotakiwa.
Malezi, Makuzi, Mafundisho Kurithi Jambo vyaweza kuwa ni moja ya vigezo vinavyoweza kupelekea Tatizo La kutoa harufu Mwilini.
Labda Tuanze Kuangalia zile sehemu zinazosifika Zaidi kwa kutoa Harufu Mbaya Hasa Kwa Kina Dada Sababu zinazoweza kusababisha na njia za kawaida kuepukana na tatizo hilo.
[divider]KINYWA:[/divider]
SABABU ZA KUTOA HARUFU MBAYA YA MDOMO ZINAWEZA KUWA ZINATOKANA NA KUTOSAFISHA KINYWA CHAKO VIZURI, HEBU JIULIZE MTU ANAPIGA MSWAKI KWA DAKIKA TATU AU MBILI KAMALIZA KWELI UNAUHAKIKA UTAKUWA UMESAFISHA KINYWA CHAKO VIZURI NA KUSUGUA KILA PANDE YA MDOMO KWA MFANO PANDE ZOTE ZA MENO, ULIMI UKAUSUGUA VIZURU IKIWEZEKANA HATA URUDIE MARA MBILI UPANDE WA JUU WA KINYWA KWENYE MASHAVU NK? KISHA UKASUKUTUA KWAMAJI SAFI NA SALAMA?
SWALA LA KUSAFISHA KINYWA SI SWALA LA DAKIKA KADHAA UMEMALIZA NI SWALA REFU KULIKO HATA KUOGA, HAKIKISHA KINYWA CHAKO NI SAFI ULIMI WA MWANADAMU HAUTAKIWI KUWA MWEUPE HAPO MAANA YAKE NI MABAKI YA MLO UNAKULA RANGI INAYOTAKIWA NI PINK, JITAHIDI KUSAFISHA KINYWA CHAKO HATA MARA MBILI KWA SIKU USIACHE KUSAFISHA KINYWA PINDI UNAPOHITAJI KWENDA KULALA.
UNAWEZA KUSAFISHA KINYWA LAKINI BADO UKAWA UNATOA HARUFU MBAYA MDOMONI.
HAPA TATIZO NI MFUMO NA UTARATIBU WAKO KATIKA SWALA ZIMA LA LISHE YAKO, TUSILE ILIMRADI KULA NA KUJAZA TUMBO, TULE KWA AFYA NA TUZINGATIE KANUNI ZA MLO ILI KUUFANYA MFUMO WA USAGAJI MWILI KUKISAGA CHAKULA KWA WAKATI NA KUTENGANISHA UCHAFU NA KILE SALAMA KWA AJILI YA MANUFAA YA MWILI SASA ULAJI WETU UNAWEZA KUWA TATIZO MARA MFUMO WA USAGAJI UNAPOKUWA HAUTEKELEZEKI KWA WAKATI MAANA YAKE MLUNDIKANO WA UCHAFU AMBAO ULITAKIWA UTENGWE NA UPELEKWE KATIKA NJIA YAKE UTOKE KAMA KINYESI UNABAKI TUMBONI MAANA YAKE NI KWAMBA HARUFU ITATOKEA MDOMONI HATA UPIGE MSWAKI MARA MIA KWA SIKU (HII HATA KWA WANAUME) JITAHIDI KULA KWA WAKATI,
KULA VYAKULA LAINI USIKU KWASABABU USIKU HAKUNA SHUGHULI ITAKAYOUPA MFUMO WA CHAKULA KUSAGA CHAKULA KWA UFANISI HIVYO UNASHAURIWA KULA VYAKULA LAINI, LAKINI PIA KUMBUKA KULA MATUNDA KAMA MAPAPAI NDIZI KWA WANYWAJI WA VILEO ILI KUSAIDIA KUSAFISHA TUMBO, KATIKA HALI YA KAWAIDA MWANADAMU ANATAKIWA APATE CHOO ANGALAU MARA MBILI KWA SIKU SASA KAMA UNATATIZO LA KUTOPATA CHOO NI TATIZO NA NIMOJA PIA YA TATIZO LINALOWEZA KUKUSABABISHI HARUFU MBAYA YA MDOMO.
KUNYWA MAJI ROBO SAA AU NUSU SAA BAADA YA MLO ILI KUPISHA MFUMO WA USAGAJI UFANYEKAZI YAKE KABLA HUJACHANGAMYA HABARI NA UKAVURUGA MFUMO HATIMAE CHAKULA KISISAGIKE UNYWAJI WA VILEO, UVUTAJI SIGARA PIA YAWEZA KUWA SABABU NYINGINE YA KUKULETEA HARUFU MBAYA MDOMONI KAMA HUTAZINGATIA USAFI WA KINYWA MARA BAADA YA KUTUMIA. KUNYWA MAJI MENGI BAADA YA KILEO OSHA MDOMO AU TUMIA PIPI AU BIG G BAADA YA KUVUTA SIGARA TUMIA MOUTH WASH JITAHIDI KUTOA NYONGO ASUBUHI BAADA YA KUTUMIA KILEO CHUKUA MUDA KUSAFISHA KINYWA CHAKO.
[divider]KWAPA[/divider]
KUNABAADHI YA WATU WANAAMINI KUWA KUTOA HARUFU YA KIKWAPA NI UGOJWA LA HASHA, NA HII NI KWASABABU ANAYETOA HARUFU HAJISIKII ILA WA PEMBENI NDIO HUSIKIA LAKINI INAKUWA NGUMU KUELEZANA UKWELI PALE INAPOJITOKEZA NA KUBAKI KUSEMANA PEMBENI HAIPENDEZE? NI NGUMU KWELI LAKINI KUNA NJIA ZA KUMFANYA KUMSAIDIA MTOA HARUFU ASIENDELEE KUAIBIKA NA HILO.
KAMA HUTAOGA NA KUJISUGUA VIZURI KWA DODOKI AU BRUSH BASI UTAKUA NA NONGO ITAKAYO GANDA SIKU HADI SIKU KUTOKANA NA MAVUMBI NA MAFUTA UNAYOPAKA NA KUSABABISHA UTOE HARUFU HATA KAMA UNAOGA KILA SIKU, NI LAZIMA KUJISUGUA EIDHA KWA KUTUMIA KITAMBAA, BRUSH DODOKI AU KITU CHOCHOTE AMBACHO UNAHISI KITASAIDIA KUTOA NONGO INAYOGANDA MWILINI VINYWELEO VIATUSAIDIA KUFANYA NGOZI IPUMUE KWA KUTOA UCHAFU WA JASHO MWILINI SASA KAMA VINYWELEO VITAZIBA KWASABABU YA UCHAFU THEN HAUTATOKA NJE NA UTABAKI KWENYE NGOZI NA MWISHO UTAJIKUTA UNATOA HARUFU HATA WAKATI MWINGINE KUTENGENEZA VILPELE VIDOGO VIDOGO (RASHIAZ) VITAKAVYOHARIBU HATA NGOZI YAKO KWASABABU YA KUSHAMBULIWA NA BAKTERIA WA UCHAFU,
HIVYO HAKIKISHA UNAJIOGESHA KWA MAJI MENGI NA SABUNU YA KUTOSHA HUKU UKITUMIA KISUGULIO KATIKA KILA SEHEMU YA MWILI WAKO, TUMIA DEODORANT AU KAMA NI GHALI TUMIA NDIMU HUWA INAKATA JASHO LA MWILI MARA BAADA YA KUOGA NA JITAHIDI KUOGA ANGALAU MARA MBILI KWA SIKU BILA KURUDIA NGUO KUANZIA ZA NDANI MPAKA ZA NJE,
USIPAKE MANUKATO (PARFYUM ) KWENYE MAKWAPA SI SEHEMU YAKE HUKO PANAHITAJI DEODORANT AU BODY SPREY USISAHAU KUNYOA NYWELE ZA KWENYE MAKWAPA YAKO KILA MARA UONAPO ZINA KUA KUNA NJIA NYINGI YA KUZITOA UNAWEZA TUMIA WAX, SHAVING MACHINE, CREAM ZA KUTOLEA VINYWELEO NK
[divider]UKE[/divider]
TATIZO LA KUTOA HARUFU UKENI LAWEZA ANZA TANGU UTOTONI KAMA MZAZI HATAKUWA MAKINI KATIKA USAFI WA MTOTO WA KIKE, MTOTO WA KIKE NI MTU SENSITIVE SANA ANAHITAJI USAFI WA HALI YA JUU TANGU KATIKA KIPINDI CHA UTOTO.
WAZAZI WENGI WAMEKUWA WAVIVU KATIKA KUZINGATIA SWALA LA USAFI KWA WATOTO WAO HASA WA KIKE HUWEZI KUMUACHA MFANYAKAZI AKAKUOSHEA MTOTO WAKO MIAKA YOTE, UNAUHAKKA GANI ANAMSAFISHA INAVYOTAKIWA? KAMA MAMA AU MLEZI UNAPASWA KUMUOSHA MTOTO WAKO NA UNAPOONA ANAANZA KUKUA NA KUPATA AKILI UNAKUWA UNAMFUNDISHA NAMNA ANAVYOTAKIWA KUJIOSHA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, SEHEMU ZA SIRI ZA MTOTO WA KIKE ZINA MIKUNJO MINGI SANA UNATAKIWA UZICHAMBUE KWA KUZISUGUA KIDOGO KIDOGO KWA KITAMBAA LAINI BILA KUMUUMIZA MTOTO KUTOKANA NA ULAINI WA SEHEMU ZENYEWE LAKINI UTAKUTA MTOTO MDOGO ANATOA HARUFU UKIMSOGELEA AU UKIANGALIA NGUO YAKE YA NDANI INAOTA UKUNGU KATI KATI ULE NI UCHAFU.
MFUNDISHE KUJISAFISHA KILA MARA AENDAPO HAJA KWA KUZINGATIA KANUNI ZA KUJISAFISHA UKENI WAKATI WA KUJISAIDIA KAMA KUJIOSHA UKE KABLA SEHEMU YA HAJA KUBWA ILI KUZUIA KINYESI KUJA MBELE WAKATI WA KUJISAFISHA JAMBO LINALOWEZA MSABABISHIA MAGOJWA KAMA INFECTION AU UTI, WENGI HAWAJUI UTI NI UGOJWA UNAOLETWA NA BAKTERIA WACHAFU KWA KUTOKUZINGATIA USAFI NA UMAKINI KAMA HIVYO, KUVAA NGUO YA NDANI YENYE UNYEVU UNYEVU, KUTUMIA PEDI KWA MUDA MREFU, KUSHIKA MLANGO WA CHOO BILA KUJUA ALIYETANGULIA ALIUSHIKA AKIWA KATIKA HALI GANI KISHA UKAJISHIKA SEHEMU ZAKO ZA SIRI WAKATI WA KUNAWA, KUTUMIA MAJI YALIOKAA MDA MREFU MSALANI AU TOILET PAPER LAKINI MARA INGINE HATA VYOO VYA SHIMO HAPA MAJIVU YANASAIDIA UKIWA UNAMWAGA MARA KWA MARA KAMA NI MTUMIAJI WA AINA HIYO YA VYOO JITAHIDI KUTEMBEA NA WET TISSUE ILI ZIKUSAIDIE UNAPOHITAJI KUJISAIDIA KATIKA VYOO VYA JUMUIYA.
KWA WASICHANA WAKUBWA AMBAO SIO BIKRA TENA WANAWEZA KUJIOSHA KWA KUINGIZA KIDOLE CHAKE NDANI YA UKE NA KUTOA UCHAFU UNAOZALISHWA HUMO IKIWA NI HALI YA KAWAIDA KILA AOGAPO NA KUHAKIKISHA ANATOA UCHAFU WOTE HATA PALE ANAPOTAKA KUINGIZA TENA KIDOLE KINAKWAMA HIYO INAASHIRIA USAFI UMETOSHELEZEA, PEMBENI YA MASHAVU YA UKE NDIO KUNA HARUFU ZAID SUGUA KWA SABUNI MARA NYINGI MPENDE KUTUMIA MEDICATED SOAP NA MAJI SAFI AU TUMIA DETAL HIZI ZINASAIDIA KUKUKINGA NA BAKTERIA WAHARIBIFU.
USIJISKIE AIBU UNAPOPATA MIWASHO SEHEMU ZA SIRI NI HALI YA KAWAIDA NA INAWATOKEA WANAWAKE WENGI TU NA KUNA DAWA ZA KUTIBU, MARA NYINGINE UNAWEZA PATA MUWASHO WA KAWAIDA UNAOSABABISHWA NA SIKU UKIKARIBIA HEDHI AU UKIMALIZA LAKINI UNAWEZA KUWA NA FANGAS WANAOSABABISHWA NA MATUMIZI YA CONDOM KAMA MAFUTA YAKE HUJAPATANA NAYO, MAAMBUKIZI TOKA KWA MPENZI WAKO, VYOO TUNAVYOTUMIA, AU HATA MAZINGIRA YA MAJI UNAYOTUMIA AU UNYEVU WA NGUO ZAKO ZA NDANI HAPA TUKUMBUSHANE FUA NGUO ZAKO ZA NDANI ANIKA JUANI ZIKAUKE KABISA KISHA ZINYOOSHE ZIWE KAVU CREAM ZA KUKUTIBU FANGASI ZINAPATIKANA MADUKA YA DAWA ILA NI VIZURI UNAPOPATA MUWASHO UKAMUONA DAKTARI KWASABABU SEHEMU HIZO SIO ZA KUCHEZEA NI LAZIMA UTUMIE DAWA KUTOKANA NA MASHARTI YA DAKTARI MARADHI MADOGO MADOGO UNAYOYAZEMBEA HUWEZA KUKULETEA MADHARA MAKUBWA KATIKA MFUMO WAKO WA UZAZI HATA KUKUSABABISHIA UGUMBA AU CANCER HIVYO USIZEMBEE KWA MAANA UWEWE WAKO UPO HUMO.
JISAFISHE VIZURI KWA KUTOA UCHAFU WOTE NDANI YA UKE WAKO MARA BAADA YA TENDO LA NDOA (SEX) NA UBAKI MSAFI HAKUNA MARASHI YA KUTUMIA KUKATA HARUFU YA UKE ZAIDI YA USAFI, KUNA VITU KAMA UDI BAADHI YA WATU HUTUMIA ILA KAMA UMCHAFU NA UNATOA HARUFU HATA HUO UDI UTABAKI KUWA KICHOCHEO CHA HARUFU HIYO MBAYA NOTE MTU ANAYETOA HARUFU HUWA HAJISIKII, HIVYO UNAWEZA KUHISI HUNA HILO TATIZO LAKINI UKWELI NI KWAMBA WENZIO WANAKUSEMA PEMBENI JITAHIDI KUZINGATIA USAFI WA MWILI WAKO MARA ZOTE KUEPUKANA NA FEDHEHA HIYO.
[divider]NOTE[/divider]
TUNAOMBA WAPENZI WETU MTUAMBIE KWA LUGHA NZURI AU KWA ISHARA ILI TUSIJISIKIE VIBAYA LAKINI PIA MASHOGA KAMA MNAPENDANA KWA DHATI BASI AMBIANENI KWA NJIA SAHIHI SIO KUSEMANA PEMBENI NA TUTAKAOMBIWA TUSIJISIKIE VIBAYA KWANI ANAYEKUAMBIA USONI ANAKUPENDA KULIKO ATAKAYEKUSEMA PEMBENI
IMEANDIKWA NA: SALMA MSANGI
4 Comments
Thanx salma,,umesaidia wengi,,nakazia kwenye kujisafisha baada ya haja kubwa,hapo wadada weng wanazoa uti na magonjwa mengine bila kujua,,wakiosha nyuma wavuta mikono paka mbele,,chonde wadada,,ni hatari,,
Hiyo point salma kwani kuna cku moja nikiwa na mchuchu flani tukiwa tunavunja amri ya sita nikataka kujifanya fundi wa kuzama chumvini ila kilichotokea siwezi sema hadharani
Hi sorry naomba number yako nataka tuongee kuhusu tangazo la biashara
nimekutumia email