
Msanii mkali katika gemu la Hip Hop Ongea Na Mshua Songstress, repa kutoka Mbeya Izzo Biznezz amesema anatoka na bidhaa zake baada ya kuwa msanii tu kitu ambacho ndo alijulikana nacho bila kuwa na bidhaa.
Izzo Akiwa Na Watangazaji Wa DalaDala Beats Tee Jay Na Jj
Kwa sasa Izzo Biznezz ameamua kutoka na bidhaa kama T-shirts, kofia, flash, viatu na vitu vingine.
Akipiga stories kupitia Magic FM Dala Dala Beatz na TJ na Jimmy J Izzo aliulizwa inakuwaje kwanini bidhaa za Kibongo haziendi nje siku moja akaonekana Lil Wayne au J.Cole amevaa tisheti za Kibongo kama ilivyo sisi tunavyofanya Bongo, tunavaa sana bidhaa zao.
Sio kwamba kule nje hawaangalii Bongo wanaangalia ila inabidi tujitangaze zaidi kupitia mitandao ya kijamii zitawafikia tu, mfano Beyonce ameonekana amevaa tisheti ya msanii kutoka Afrika kusini, huo ni mfano kwamba pia kule nje wanatuangalia ila ni sisi kujitangaza zaidi…Alisema Izzo.
Akiongelea ngoma yake ya Walala hoi Izzo aliulizwa hajakutana na magumu yeyote kutokana na wimbo huo, izzo alisema hakuna magumu kwa sababu wimbo huo ni wal kila mtu kwa sababu Watanzani wengi ni masikini kwani takwimu zinaonyesha kuwa Watanzania wanakula mlo mmoja kwa siku.
Ameomba mashabiki wake kusupport ngoma hiyo ili ishike chart za Magic FM kuanzia namba 20 hadi 1 katika Chart za Bamiza.
