
Jumla ya nyumba 265 katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro zimeezuliwa paa na nyingine zimebomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Taarifa hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya hai Bwana Melkzedeki Humbe wakati wakipokea msaada wa chakula na mabati ,kutoka kampuni ya vinywaji baridi ya bonite bottlers limited ya mjini Moshi.
Humbe amesema, kaya 1005 hazina makazi wala chakula, baada ya nyumba zao kuezuliwa paa na nyingine kubomoka kutokana na upepo na mvua iliyonyesha, hivyo kuharibu chakula walichokuwa nacho, mashamba, majengo ya shule, miundombinu ya barabara na nguzo za umeme katika baadhi ya maeneo.
