
Mkali anayetokea Compton The baddest rapper Kendrick Lamar amewapa mashavu Jay Z, Nas,Dr. Dre kwa kuwa imara na bado kuendelea kuupenda muziki.
Kendrick alisababisha maneno kibao baada ya kujitangaza kama Mfalme wa New York kwenye lines zake za wimbo wa “control” wa Big Sean karibu mwaka mmoja uliopita..
Kendrick aliongelea Ufalme wake wa New York ikiwa sehemu ya story kwenye gazeti la Complex.
Kendrick hakuwa na mengi ya kusema lakini aliwaongelea wakali wa mistari ambao anaamini ni Wafalme wa New York.
.”Nampenda B.I.G na Jay wataendelea kuwa Wafalme wa New York” alisema Kendrick Lamar
“Hii kiukweli ni Baraka kutoka kwenye nguvu zaidi, Ingawa naelewa kwamba hakuna mipaka kwa kile nachokifanya, kila kitu kipo mbele na wao, nikiwa studio na natafuta ubunifu bado sijafanana tayari, kitu ambacho sijawahi kukihisi, ni juu sana. Nikiwaangalia Jay Z, Nas, Dr. Dre hawa watu walianza lakini wanaupenda muziki na wanaupenda kupita kiasi kila wakati unataka hisia hiyo ya ubunifu” aliongeza Kendrick.
