
Habari ya Jay z na Beyonce kufanya albamu ya pamoja ilitoka siku tu baada ya tour yao ya mwisho ya “On The Run” huko Paris wikiendi iliyoisha Septemba 13.
Jay z na Beyonce wameshaanza kurekodi albamu hiyo ya pamoja amesema DJ Skee.
DJ Skee alitangaza habari hiyo juzi kati wakati wa uzinduzi wa Dash Radio na alisema amethibitisha taarifa hiyo na zaidi ya chanzo kimoja.
Tour yao ya bara la Marekani ya kusini peke yake imeingiza zaidi ya dola milioni 100 taarifa za Billboard zimeeleza, Mwezi Agosti Billboard ilitoa taarifa ikikadiria kuwa kwa show moja tu walitengeneza dola milioni 4 ikiwa na maudhurio ya watu 45,000 kwa show, Tour ya Marekani ya kusini inakadiriwa kuwa ilihudhuriwa na watu 850,000 kwa show 19 zilizofanyika.
Show mbili za mwisho katika tour hiyo huko Paris imerekodiwa na itarushwa ikiwa sehemu maalum ya concert hiyo imepangwa kuonyeshwa Jumamosi Septemba 20, Juzi Jay z na Beyonce walitoa sehemu ya kwanza ya sehemu maalum ya tatu inayoitwa “Bang Bang”.
