Ukiongelea tasnia ya muziki nchini Tanzania hususani Bongo Flava, jina Lady Jay Dee linasikika kichwani kwako linaita Ndi “Ndi Ndi” LOL, majina yake mengine ni Mama Some Food, Binti Machozi, Commando Jide, tuache majina kwa sababu unaweza ukataja majina ukajaza ukurasa mzima, jina lake halisi ambalo lipo kwenye passport ni Judith Wambura.
Lady Jay Dee ni mwanamuziki wa kike katika Bongo Flava ambaye amevuka mipaka ya rika, yani anasikilizwa na wazee, wakinamama, vijana na watoto kutokana na aina ya muziki anaoimba. Katika mitandao mengi yamekuwa yakiongelewa juu ya aina ya muziki anaoufanya, kuanzia maudhui, midundo yake na sauti yake inayosikika bila kuchosha akili ya msikilizaji, Lady Jay Dee ana utambulisho wake (very stong Identity) ukisikia tu unajua huyu ni Lady Jay Dee.
Ni mwanamuziki ambaye ukifuatilia historia ya muziki wake, wasanii wote aliofanya nao wimbo wa kushirikiana nyimbo hizo zote zilikuwa hit, mfano ‘Machoni Kama Watu’ ya A.Y, ‘Single Boy’ ya Alikiba, ‘Alikufa Kwa Ngoma’ ya Mwana FA “Msiache Kuongea” akiwa tena na Mwana FA na nyingine kibao endelea mwenyewe kuzikumbuka, hizo ni baadhi lakini zipo zaidi ya nyimbo 10 alizoshirikishwa zikawa.
Nyimbo zote za Lady Jay Dee huwa ni stori kuhusu maisha yake, haya ni maneno ambayo kila mtu anasema mtaani, kabla ya kuandika stori hii rafiki yangu anayeitwa Jackson alisema hili katika group moja nililopo, lisemwalo lipo kama halipo linakuja.
Maisha yake anayoyaongelea ndo huwa maisha kwa ujumla ya kila mtu, ni mambo ambayo yanatokea kwa binadamu wote, nyimbo zake ni somo, pia huwatia watu moyo wa kuendelea kusonga mbele, amekuwa mfano katika jamii, hata kupewa jina la Commando.
Wakati wimbo wa ‘Ndi Ndi Ndi’ umetoka imeonekana kwa asilimia kubwa watu wengi wameuelewa, wimbo huu ukiwa na siku mbili tu toka utoke, ukisikiliza wimbo wa ‘Ndi Ndi Ndi’ ni muendelezo wa stori za maisha yake.
Hivi karibuni Lady Jay Dee ilitangazwa ameachana na mume wake ambaye ni Mtangazaji maarufu hapa nchini Bw. Gadner G. Habash amabye kwa sasa ni mtangazaji wa redio E.FM 93.7 Dar es salaam, mengi yakasemwa lakini yamepita, endelea kusikiliza ‘Ndi Ndi Ndi’ kwa asilimia hata 2.01, Lady Jay Dee ameongelea maisha yake ya mpaka sasa, ‘Hatua kwa hatua ngazi nazipanda, nayo makovu yameniimarisha’ anasikika anaimba Lady Jay Dee kwenye wimbo wa ‘Ndi Ndi Ndi’.
Unaonaje kama Lady Jay Dee na Gadner kuachana kwao ingekuwa ni maagizo ili biashara ifanyike? kwa sababu bila ya kuachana na Gadner angeimba nini? Wengi walitamani sana kumsikiliza Lady Jay Dee ataimba nini baada ya kuachana na mume wake ambaye rumors has it kwamba alimpenda sana.
Kama kawaida ameendeleza kwa kiasi fulani stori, hapa ndipo unapogundua Lady Jay Dee ni mwanamuziki ambaye anaishi maisha ya tofauti sana.
Lady Jay Dee na Gadner kama wanaigiza kuachana ili wafanye biashara basi wamefanikiwa sana, na mashabiki wanaomba iwe hivyo, Lady Jay Dee na Gadner kama wajaachana itakuwa prunk ambayo haijawahi kutokea kwa sababu ina chembechembe kana kwamba sio kweli wameachana, watu wanaruhusiwa kuwaza wanavyowaza, utafiti mdogo unaonyesha kwamba Lady Jay Dee na Gadner ilikuwa couple inayotazamwa sana, na yenye nguvu.
Lakini sio Tanzania tu, hata mastaa wa nje, mastaa ambao ni maarufu wakioana huwa hawadumu sana wengi huachana.
Lady Jay Dee ni msanii wa kike ambaye ameshinda tuzo mbalimbali barani Afrika ikiwemo ya KORA pamoja na za nchini Tanzania za Kilimanjaro Tanzania Music Awards, akiweka historia ya msanii ambaye hajawahi kupokea tuzo yake huwa anapokelewa na mwakilishi na hii ni kitu ambacho kinaongeza utofauti kwa mwanamama Lady Jay Dee.
Chanzo: see the africa link