Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family Said Fella amesema mahusiano yake na msanii wa kundi la TMK Wanaume Halisi Juma Nature wao hawahusiani kwenye kazi tu mfano kumsimamia kazi zake za kimuziki lakini kwenye mambo mengine wao ni waskaji wanaongea na kushirikiana. Fella alisema hayo wakati akipiga stories na Dala Dala Beats ndipo alipoweka wazi hayo.
Haya yote yamekuja kufuati Mkubwa Fella na Juma Nature walipoonekana pamoja kwenye kumuaga msanii aliyefariki wa kundi la TMK Wanaume Family marehemu Y.P, watu wengi walidhani kwamba Juma Nature na Said Fella hawapatani wala hawaongei lakini, Fella ameweka sawa na ametaka mashabiki wajue kwamba wao ni washkaji na wanaongea ila tu Fella ndo hasimamii kazi za Nature kama ilivyokuwa awali kabla kundi hilo halijatengana mwaka 2010 na kufanya kuwa na makundi mawili ya TMK Wanaume Family na TMK Wanaume Halisi kundi ambalo linaongozwa na Juma Nature.
Itakuwa fresh sana siku moja Fella wakawa pamoja kikazi na Juma Nature kwa sababu Nature pindi anapokuwa anasimamiwa na Fella huwa anafanya vizuri sana kutokana na management ya Fella.
salmamsangi.com inawapa pole watu wote walioguswa na msiba huo wakiwemo wasanii wote, ndugu, jamaa na marafiki.