Msanii wa Filamu Nchini Kajala Masanja ameamua kufunguka na kutoa ya moyoni baada ya kuchoshwa na uzushi ulioenea sana juu ya mahusiano yake na mume wa mtu..
Kama Binaadamu Kajala amekiri kuumia na kuchoshwa na uzushi huo ambao kwa mujibu wake si kweli
Kumekuwa na Uzushi wa siku nyingi kuwa Msanii Kajala Masanja anajihusisha kimapenzi na Mume wa Mmiliki wa Blog Ya 8020 fashion Shamim Mwasha, Abdil Nsembo Jambo ambalo Kwa Mujibu Wa Kajala Si kweli,
Shamim Akiwa na Mumewe Abdul Nsembo
Hata Hivyo kajala alionyeshwa kushangazwa na uzushi huo ambao hata hajui chanzo chake
Kajala aliamua kuyatoa ya moyoni kupitia ukurasa wake wa picha wa Insta Gram kwa kuandika
“NADHANI NAMJUA HUYU DADA SIKU NYINGI SANA,KABLA HATA YA WENGINE WENU KUMJUA TUNAHESHIMIANA SANA NA HATUJA WAHI KUKOSEANA SASA SIJUI NANI ALIYEANZISHA HABARI YA MIMI NATEMBEA NA MUME WAKE NA SIJUI ALIFANYA HIVYO KWA MAKUSUDI GANI NAUMIA KILA SIKU KWA AJILI YA UJINGA WA WATU NA HAYO MAGAZETI NIKIWAAMBIA NIPENI USHAHIDI YA KUWA NATEMBEA NA MUME WA SHAMIM SIJUI MTAFANYA DAH… SIJUI NISEME NINI @8020FASHION MPZ ENJOY NA NDOA YAKO ACHANA NA WAPUMBAVU NIMEVUMILIA NIMEONA LEO NIANDIKE UNAJUA SIPENDAGI KUONGEA LAKINI GAZETI LA JANA LIMENIKWAZA SANA” Mwisho wa kunukuu