Siku ya jana Jumatano 7, 2014 mjini Dodoma ilikuwa ni siku ya kihistoria baada ya katiba inayopendekezwa kukabidhiwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dokta Shein.
Mwakilishi wa wasanii Saimon Mwakifamba akizungumza alisema katiba hii inayopendekezwa ni katiba ambayo imewamulika wasanii kwa eneo kubwa kitu ambacho ni historia kwani katika katiba ya sasa wasanii waliachwa nyuma na kuwafanya kuwa katika mazingira magumu.
Katiba inayopendekezwa kwa sasa ni katiba bora ambayo kama ikipita wasanii wataona manufaa ya katiba hiyo.
Saimon Mwakifamba alikuwa ni mmoja wa wajumbe katika bunge maalum la katiba ambapo alikuwa akiwakilisha wasanii wote kwa ujumla.
Wajumbe wamefanya kazi kubwa kuitengeneza katiba hiyo pendekezwa, na baada ya hapo katiba hiyo pendekezwa italetwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya hapana au ndio ili iweze kuwa katiba kamili.
Wananchi wamesisitizwa kusoma katiba hiyo pendekezwa kwa makini na kuielewa, wasisomewe na kuambiwa kipi cha kufanya wafanya maamuzi yao binafsi lakini sio kushikiwa akili ili kupata katiba bora ambayo itamkgusa kila mmoja katika sekta mbali mbali.
Katiba Inayopendekezwa Yakabidhiwa Kwa Rais, Kwa Mara Ya Kwanza Ikiwa Imewamulika Wasanii Kwa Kiasi Kikibwa
Previous Story
Rick Ross Asema Yuko Kichwani Mwa Jay Z Na Diddy
Related Posts
-
-
@The_Dati Kutua Universal Music London Mwezi Machi
-
East Africa Beach Party @ Azura Beach Mikocheni 1 Day 2 Go!! Get Ready
-
Forbes List Ya Mastaa Wenye Mkwanja Mayweather Ashika Nafasi Ya 7
-
Usher Raymond Amemsaidia August Alsina Kwa Sababu Pia Yeye Alisaidiwa
-
Keeping Up With Kim? Picha Zinaonyesha Jinsi Kylie Jenner Anavyomcopy Dada Yake
-
Picha:Uzinduzi wa Video Ya Diamond Platnumz Serena Hotel