“Huu muziki ni kitu ambacho dunia inatakiwa kusikia na sio kwa ajili yangu tu lakini ni kwa ajili ya vitu vinavyoumiza kichwa (stress) ni kwa ajili ya maisha yetu” alisema Kendrick a.k.a K.Dot.
Wimbo wa Kendrick Lamar wa “I” imetoka Jumanne Septemba 23 lakini msanii huyo anasema haoni kama wimbo huo uitwe wimbo.
“Nataka niondoe neno “single” , nataka kuita ngoma nazoachia “statements” kwa sababu huu muziki ni kitu ambacho dunia inataka kusikia na so kwa ajili yangu tu, na kwa ajili ya stress, ni kwa ajili ya maisha yetu, naporudi kwenye kuachia ngoma, nataka nihakikishe nafanya hivyo tu na kuendeleza hilo” alisema Kendrick Lamar wakati akipiga stories na redio ya Los Angeles Power 106 na Jeff G.
Wakati wa mahojiano na AMP Radio ambayo ilifanyika Jumanne, repa huyo kutoka Compton California alisema kwamba alijaribu kupunguza muziki wa msukumo wa nje wakati akifanyia kazi albamu yake inayokuja.
“Napokwenda kutengeneza albamu au aina yeyote ya wimbo, naacha kila kitu kutoka kwenye redio kwa sababu unaweza ukashawishiwa na nyimbo zile unazozipenda, nyimbo ambazo huzipendi, kwa hiyo nilisema nitakwenda studio na nitafanya kitu ambacho hakishawishiwi na mambo yanayoendelea sasa hivi katika kiwanda cha muziki au kitu ambacho watu wanatabiri nitafanya, kwa sababu mwisho wa siku, mimi ni msanii na nitachukia kila siku kufanya kitu kinchofanana” aliongeza Kendrick Lamar.
Kendrick Lamar Ataka Ngoma Zake Ziitwe “Statements” Sio “Single”
Related Posts
-
-
Rapper 50cent Asema Mama Wa Mtoto Wake Ndio Chanzo Cha Habari Za Yeye Kutohudhuria Mahafali Ya Mwanae Kusambaa…. Aleza Sababu
-
Rihanna Kawa Muislam??? Aonekana Msikitini Huko Abu Dhabi .
-
M TO THE P ALIYEKUWA NA NGWEA NAYE AFARIKI DUNIA LEO
-
Tecno Afuta Picha Zote Za Instagram Zinazomwambia R.I.P Kutoka Kwa Mashabiki Wa Tanzania
-
Breaking News: Dina Marious awa Mwanamke wa mwaka
-
Lil Wayne Kuja Na Tour Inayoitwa Drake Vs Lil Wayne